Mateso ya wahamiaji Libya yafichua utepetevu wa Umoja wa Mataifa
Huwezi kusikiliza tena

'Wateswa na kudhulumiwa’: Kisa cha mwanamke wa Kisomali Libya

Baada ya miaka miwili ya mateso kupitia mataifa matatu- kununuliwa na kuuzwa na walanguzi wa watu na boti kuishiwa na mafuta akijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean - Mohamed hatimaye alipoteza matumaini.

Mke wake Leyla aliye na miaka 21, anakumbuka siku aliyojichoma moto baada ya kugundua hawakujumuishwa katika orodha ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa.

Alipelekwa katika kituo cha Triq al-Sikka cha kuwazuilia wahamiaji na wakimbizi kinachoendeshwa na waasi wanaounga mkono serikali mjini Tripoli na kupewa msaada wa kibinadamu.

(Jina lake halisi limebadilishwa kutokana na sababu ya usalama wa Leyla.)