Kwanini wanaharakati waanzisha kampeni kwa niaba ya Kabendera?

Erick Kabendera

Kampeni imeanzishwa katika mitandao ya kijamii hii leo Tanzania kwa anuani ya #100K4Erick iliyonuiwa kuonesha kumuunga mkono mwandishi wa habari nchini humo Erick Kabendera.

Kabendera alishtakiwa hapo jana katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kwa tuhuma za ubadhirifu wa kiuchumi.

Kampeni hiyo infanyika katika wakati ambapo kumekuwa na wasiwasi ndani na nje ya Tanzania kuhusu namna ambavyo amekamatwa, na taswira inayotokana na hatua hiyo kwa uhuru wa yombo vya habari nchini humo.

Pia baadhi ya wanaharakati wameonyesha kushangazwa na kubadilika kwa yaliominika kuwa ndio makosa anayotuhumiwa nayo.

Awali maafisa wa polisi na wale wa idara ya uhamiaji walisema anachunguzwa kuhusu utata wa uraia wake.

Siku ya Ijumaa mawakili wake walitoa taarifa wakieleza mteja wao atashtakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapiswha katika jarida la The Economist.

Hapo jana alishtakiwa kwa makosa matatu, anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania.

Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.

Image caption Kabendera akishauriana na wakili wake Jebra Kambole katika mahakama ya Kisutu

Makosa hayo hayana dhamana na ataendelea kusalia rumande mpaka mwisho wa kesi yake. Agosti 19, kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mahakamani.

Mtandao wa Twitter ulitapakaa ujumbe ulioambatinisha hashtag hiyo kuanzia saa sita mchana wa leo kufuatia wito na wanaharakati wa haki za binaadamu na wa mitandao ya kijamii.

Muda wa saa sita mpaka saa nane ulitengwa ili watu wasiandike ujumbe wowote katika mitandao ya kijamii kando na ujumbe wa kuonyesha kumuunga mkono Kabendera.

Haya ndio baadhi ya yaliozungumzwa:

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii