Kasuku mkubwa zaidi duniani agunduliwa New Zealand

Wataalamu wa histoia na maumbile ya wanyama walibaini mafufu ya kasuku kusini mwanchi ya New Zealand Haki miliki ya picha PA Media
Image caption Wataalamu wa historia na maumbile ya wanyama walibaini mafufu ya kasuku kusini mwanchi ya New Zealand

Kasuku mkubwa ambaye alizurura New Zealand takriban miaka milioni 19 iliyopita alikuwa na urefu wa mita 1m (futi 3 na ichi 2 ) - kwa karibu nusu ya wastani wa urefu wa biadamu , utafiti mpya umebaini.

Masalio ya kasuku huyo yalipatikana karibu na eneo la St Bathans katika jimbo la kusini mwa nchini ya New Zealand la Otago.

Kutokana na ukubwa wake, kasuku huyo anaaminiwa kuwa alikuwa na hawezi kupaa na alikuwa hali nyama tofauti na ndege wa leo.

Utafiti huo wa ndege ulichapishwa Jumanne katika jarida la masuala ya Kibaiolojia -Biology Letters.

Akiwa na uzito wa zaidi ya kilo saba, ndege huyo angekuwa na uzito mara mbili ya kasuku aliyejulikana kama kākāpo, ambaye awali alifahamika kuwa ndiye aliyekuwa mkubwa zaidi miongoni mwa ndege wa aina hiyo.

"Hakuna kasuku mwingine mkubwa duniani ," ameieleza BBC Profesa Trevor Worthy, mtaalamu wahistoria na a maumbile ya wanyama katika Chuo kikuu cha Flinders nchini Australia na mwandishi wa utafiti huo. "Kumpata mmoja ni muhimu sana ."

Wataalamu wa historia na maumbile ya wanyama wamekiita kizazi hicho cha kasuku kama Heracles inexpectatus jina la shujaa wa kusadikika wa Kigiriki kutokana na ukubwa wake usio wa kawaida na uthabiti.

Mifupa ya kasuku huyo - awali iliaminiwa kuwa ni ya tai au bata - na ilitunzwa katika hifadhi kwa miaka 11 hadi mapema mwaka huu , wakati timu ya wataalamu wa historia ya maumbile ya wanyama walipoitambua.

Prof Worthy alisema kuwa wanafunzi wake walikutana na mifupa ya kasuku huyo kwa bahati katika maabara wakati wa mradi wa utafiti.

Haki miliki ya picha PA MEDIA
Image caption Kasuku aliyeitwa, Heracles (jina la shujaa wa kusadikika wa Kigiriki)anakadiriwa kuwa na ukubwa nusu ya binadamu

Mdomo wa kasuku huyo unaaminiwa kuwa ungekuwa mkubwa sana , Mike Archer wa chuo kikuu cha historia na maumbile ya wanyama NSW alisema, "ingeweza kupanua kinywa chake na kuingiza chochote ilichokitaka".

Profesa aliliambia shirika la habari la AFP kuwa kasuku huyo "huenda alikuwa anakula chakula zaidi ya kile anachokula kasuku wa kawaida ,au hata kuwala kasuku wengine".

Hata hivyo , kwasababu kasuku hakuwa anawindwa na wengine , huenda hakuwa mkali , Profesa Worthy ameiambia BBC.

"Huenda aliketi ardhini, kutembea tembea na kula mbegu na karanga, zaidi ," alisema.

Paul Scofield, afisa wa ngazi ya juu wa hifadhi asilia katika makumbusho ya Canterbury , aliliambia shirika la habari la AFP kwamba watafiti tulilikuwa "Tunaweka pesa zetu katika utafiti kwa ndege ambaye hapai angani".

Uvumbuzi wa ndege wakubwa sio wa kawaida nchini New Zealand, zamani ikiwa ni nyumbani kwa mbuni , ambao kwa sasa wametoweka ambao urefu wao ulikuwa unakadiriwa kuwa wa mita 3 nukta 6 (futi 11 na inchi 8 ).

St Bathans, ambako mifupa ya mguu wa kasuku mkubwa ulifukuliwa , ni eneo linalofahamika kwa kuwa na mafuvu mengi ya kale ya wanya walioishi kuanzia miaka milioni 23 hali milioni 5.3 iliyopita.

" Lakini hadi sasa, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi hata mara moja kumvumbua kasuku mkubwa - popote," Prof Worthy ameliambia shirika la AFP.

"Tumekuwa tukifufu mafuvu haya kwa miaka 20 , na kila mwaka unafichua ndege wapya na wanyama ... Bila shaka kuna jamii nyingi zisizotarajiwa ambazo zitazofufuliwakatika eneo hili la kuvutia."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii