Wafanyakazi wa Microsoft 'husikiliza' baadhi ya simu za Skype

Nembo ya app ya Skype kwenye kompyuta ya Mac Haki miliki ya picha Getty Images

Wafanyakazi wa Microsoft wakati mwingine husilikiza mazungumzo halisi ya Skype ambayo yametolewa na programu ya kutafsiri, imeelezwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya teknolojia ya Motherboard, baadhi ya wakandarasi wengine wa Microsoft wanakagua mazungumzo kama haya ili kuangalia ubora wa tafsiri.

Hatahivyo, ukweli kwamba wanadamu wanaweza kusikiliza simu hazijaelezewa wazi masharti na vigezo vya Skype.

Microsoft ilisema ina ruhusa ya watumiaji kukusanya na kuchakata data zao.

Huduma ya kutafsiri ya Skype hutafsiri mazungumzo wakati wa mazungumzo ya moja kwa moja kwa njia ya sauti au video.

Motherboard ilisema ilipata sauti kutoka kwenye mazungumzo ya Skype yaliyotafsiriwa ambayo watumiaji "walizungumza na wenza wao" na kujadili mambo ya kibinafsi, masuala ya kupunguza uzito pamoja na changamoto za mahusiano.

Namna ya kuficha mawasiliano yako kwenye WhatsApp

Imethibitishwa WhatsApp si salama

"Microsoft hupata ruhusa ya wateja kabla ya kukusanya na kutumia data zao za sauti," msemaji wa kampuni hiyo alisema katika taarifa.

"Pia tunaweka taratibu kadhaa ikiwemo kuweka kipaumbele kwa faragha ya watumiaji kabla ya kugawana data''.

Taarifa ya kampuni kuhusu faragha inasema data inaweza kugawiwa "na mawakala wanaofanya kazi kwa niaba yetu" - lakini haisemi wazi kuwa hii inaweza kujumuisha wafanyakazi binadamu badala ya, kwa mfano, mifumo ya akili ya bandia.

Haki miliki ya picha Reuters

Rekodi kupitiwa upya

Kitendo cha kutumia wakandarasi wa kibinadamu kutathmini rekodi za wateja wanaotumia bidhaa za teknolojia kumesababisha kufanyika uchunguzi hivi karibuni.

Wiki iliyopita, Apple na Google waliamua kusimamisha matumizi yao ya wakandarasi wa kibinadamu kwa kukagua rekodi za sauti zilizotengenezwa na wasaidizi wa kawaida wa makampuni pamoja na programu ya Siri ya Apple.

Siku chache baadaye, waangalizi wa data wa Luxembourg walisema kwamba imeanzisha majadiliano na Amazon kuhusu jinsi kampuni hiyo iliyoshughulika na rekodi za sauti za watu wanaotumia msaidizi wake Alexa.

Mamlaka ya usimamizi ya Microsoft kuhusu ulinzi wa data ndani ya EU ni Tume ya Ulinzi ya Takwimu ya Ireland.

BBC imeitaka tume hiyo kutoa maoni.