Betty Bigombe: Mwanamke aliyeshawishi Joseph Kony kukutana na Rais Museveni Uganda

Betty Bigombe with LRA negotiator Brig Sam Kolo (right) in 2004 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Betty Bigombe akiwa na mwakilishi wa LRA Brigedia Sam Kolo (kulia)

Betty Bigombe alikulia Kaskazini mwa Uganda na mwisho wa mwaka 1950, na aalikuwa akitembea maili nne kila siku kwenda shuleni.

Alijua kuwa kupata elimu ndio njia pekee itakayobadilisha maisha yake binafis na ya jamii nzima kw aujumla.

Miaka 30 baadae "jukumu" lake lilikuwa la kuamua hatma ya siku zijazo za eneo hilo kupita jaribio kushauriana na mbabe hatari wa kivita Joseph Kony, kiongozi wa waasi wa Lord's Resistance Army.

Bigombe alikuwa mwana wa nane kati ya watoto 11 na alikulia katika jamii utamaduni ambao unaendelea kushuhudiwa hadi wa leo.

"Bila elimu, pengine huenda nisingelikuwa hapa na huenda saa hii ningelikuwa na watoto 20 na kuishi vijijini nikifanya kazi ya malezi na zingine ngumu, kama vile kukuza chakula cha familia kwa kulima, kupalilia na kuvuna na muda huo wote pengine nikiwa nimebeba mto mgongoni huku mwingine akitambaa na pengine ningelikuwa mmoja wa wake wenza " alsema.

Familia yake ilipata msaada wa kifedha kutoka kwa kanisa wakati alipokuwa akiendelea na masomo yake.

Nafasi hiyo ilimwezesha kupata ufadhili wa elimu uliomwezesha kujiunga na Chuo Kikuu cha Harvard.

Haki miliki ya picha Betty Bigombe
Image caption Betty (kulia)na mama na dada yake

Mapema miaka ya 1980, alirejea nyumbani akiwa ameolewa na watoto wawili.

Taifa lake lilikuwa limetumbukia kwenye vita ambapo vikosi vya rais Milton Obote vilikuwa vikikabiliana na vuguvugu lililokuwa likiongozwa na Yoweri Museveni.

"Wakati huo, nilikuwa nikiwaficha baadhi ya watu waliokuwa wakimuunga mkono rais Museveni. Nilifanya kazi na mwanamke mmoja raia wa Ujerumani aliyekuwa akihudumu katika shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR na tulisaidia kuwapeleka watu waliokuwa hatariri nchini Kenya. Ukiwa na bendera ya UN, ni rahisi. tuliweza kupita vizuizi vya barabarani na kuwafikisha mahali salama. hali iliyowafanya watu kupigania haki zao."

Mwaka 1986, Museveni alikuwa rais, wadhifa anaoshikilia hadi wa leo. Alimzawadia Bigombe kwa kumfanya waziri wa serikali.

"Nilipata usumbufu sana nilipoteuliwa katika wadhifa wa uwaziri kwa sababu mawaziri wengine walikuwa wanaome. Kile walichoniaagiza kufanya ni kusoma makaratasi, kwa hiyo nilimfahamisha rais kuwa nataka kujiuzuli kwa sababu hakuona chochote cha msingi ambacho angelifanya isipokuwa kusoma vitabu wakati alitaka kufanya kazi. Rais alishangaa sana kusikia kuwa nataka kujiuzulu. Mawaziri wa Afrika hawajiuzulu, hususana wanawake,"alisema.

Kwa hivyo Betty alikuja na pendekezo la kukutana na waasi kaskazini mwa nchi baada ya mapigano kuzu ili kufahamu walichokuwa wakipigania na mahali walipoweka silaha zao.


Museveni alikubaliana na pendekezo hilo lakini akamuomba Bigombe kuwashawishi waasi kukomesha mapigano.

Ndugu jamaa na marafiki zake walihofia mpango huo ulikuwa hatari kwa maisha.

"Watu wengi waliniambia niachane na mpango huo, 'anataka ufariki.' Marafiki waliniambia, 'Hiyo si kazi ya wanawake. Kwanini amekupatia jukumu hilo? Hujawahi kuifanya.'"

Bila shaka ni wazi kuwa hakuna mtu aliyekuwa mjasiri wa kutosha kuzungumza na Joseph Kony, kiongozi wa kundi hatari la LRA.

Waasi wa LRA walimtumia Bigombe barua wakisema Museveni amewatukana kwa kumtuma mwanamke kujadiliana nao.

Walitishia kumuua lakini hakutishika - na alijitolea kuhakikisha mapigano yanakomeshwa.

Baadae walimtuma mtu aliyetekwa na kundi la Kony kuwasilisha barua ya pili ana kwa ana.

"Mtu huyo alijitokeza na sijui aliponea vipi kifo. Hakua na chanjo ya ukambi.amekatwa sehemu ya mdomo na viungo vyake na alikuwa ameloa damu.Barua inayosemekana imetumwa kwangu ilikuwa ilikuwa imejaa damu. Kwa kweli hata sikuweza kuigusa ."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joseph Kony mwaka 2006

Bila uwoga, Bigombe aliamua kumwandikia barua Kony. alimtaja kama "mwanangu" na kutumia njia za kidini kuwasiliana nae na kuomba wakutane.

Hatimae Kony alipokubali kukutana nae. Alihofia huenda akaamua kumtesa na kumuua badala kukubali atumiwe kama chambu cha kumkamata.

Kwa mara ya kwanza walipatana ndani ya kichaka kikubwa cha kuogofya.

"Alikuwa chini ya ulinzi mkali, muziki wa kidini ulikuwa ukicheza, kulikuwa na wanaume waliovalia nguuo za watawa na walikuwa wamejihami kwa bunduki. Walikuwa wakiimba muziki wa kidini, [unaosema] kwambaushetani unakaribia kuwatoka. Mandhari hayo yalikuwa ya kushangaza. Alikuwa amevalia sare za kijeshi. ALikuwa tayari kuniogofya."

Miezi 18 baada ya wao kukutana ana kwa ana mara kadhaa Kony, alianza kumuita Betty "Mummy Bigombe".

Na hatimae alikubali kutoka mwituni kufanya mazungumzo ya amnai na rais Museveni.

Haki miliki ya picha Centre of Humanitarian Dialogue
Image caption Betty akihudhuria katika mdahalo wa masuala ya kibinadamu mjini Oslo, 2018

Bigombe alienda kukutana na rais ili wakubaliane mashariti yatakayooongoza mazungumzo hayo ya amani.

Badala ya kufanya hivyo Museveni alimtishia Kony hadharani na kutangaza katika mkutano wa hadhara kuwaajitokeze mara moja la sivyo akabiliwe vikali na vikosi vya serikali.

Kony na vikosi vyakewalijibu kwa kutekeleza mashambulizi mabaya katika kituo kimoja karibu na mpaka wa Uganda na na Sudana ambapo watu 300 waliuawa kinyama.

Bigombe alijuzulu jukumu lake na kuelekea Marekani.

"Nilisikitika sana nikalia kwa machungu ndani ya ndege. Sikuamini Tulivyoshindwa kufikia amani, lakini yote haikuwa kwa ajili -nilikuwa nawahurumia watu waliokuwa wakiteseka bila sababu," alisema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mazungumzo ya Betty na waasi wa LRA Kaskazini mwa Uganda, Desemba mwaka 2004

Alirejea tena kwa masomo Chuo Kikuu cha Harvard na baadae kuajiriwa na Benki ya Dunia mjini Washington.

Asubuhi moja mwaka 2004 alilifungulia runinga kutazama yanayojiri lakini ghafla alipana na taarifa iliyobadilisha kila kitu.

Kulikuwa na tarifa katika kituo cha habari cha CNN - Kwamba waasi wa Lord's Resistance Army walivamia kambi moja ya wakimbizi na kuua zaidi ya watu 300.

"Na baada ya hapo niliona picha yangu - ikiandamana na maandishi - Mtu pekee aliyekaribia kukomesha mapigano, mtu pekee aliyekutana na kiongozi wa waasi. Ujumbe huo nilihisi ni mwito kwangu ."

Bigombe alirejea Uganda na kujaribu kupanga tena mkutano baina yake na kiongozi wa waasi wa LRA Bw. Joseph Kony.

Hata hivyo alihofia hatua ya serikali ya Uganda kufadhili mpango huo utaathiri msimamo wake kwa hivyo aliamua kutumia pesa zake binafsi.

Alitumia fedha za masomo alizokuwa amemtengea binti yake kulipa bili ya simu yake ya satellite.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Joseph Kony

Kufikia wakati huo mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai, ICC ilikuwa imemfungulia Kony mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kazi ya Bigombe ilikua msingi wa mazungumzo ya amani nchini Dudan Kusini mwaka 2006, japo yalivunjika dakika za mwisho, baada ya Kony kukataa kutia saini mkataba wa amani.

Kony na washirika wake katika kundi la Lord's Resistance Army kutokea wakati huo walipunguza shughuli zao.

Sasa imeripotiwa kuwa afya yake imezorota na jeshi lake limepungua hadi chini ya 100.

Leo hii Bigombe ni Mkurugenzi wa kitengo cha kushughulikia mizozo katika Benki ya Dunia.

Anazuru maeneo tofauti duniani kutoa mafunzo kwa wapatanishi na kuwafahamisha alichojifunza alipokutana na waasi wa LRA mwituni.

"Hivi karibuni nilikutana na mmoja wa wapiganaji. Wao hunitafuta. Inashangaza lakini wanafanya hivyo. Miezi kadhaa iliyopita mmoja wao aliwasiliana nami na kusema, 'Mara hii Konyanataka kukutana na wewe.' Nikasema, 'Naomba uwache utani, kama kweli anamaanisha alichosema mwambie anipigie simu, Naweza kung'amua sauti yake.'"

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii