Programu ya Whatsapp inayokuruhusu kuingilia ujumbe wa watu

Whatsapp Haki miliki ya picha REUTERS

Programu mpya iliyotolewa ambayo inaweza kutumia udhaifu uliopo katika mtandao wa WhatsApp unaomilikiwa na kampuni ya Facebook inakuruhusu wewe ''kuweka maneno katika kinywani mwa watu ", Wanasema watafiti.

Timu ya ya wataalamu wa kampuni ya usalama wa mtandao Checkpoint imeonyesha jinsi programu hiyo inavyoweza kutumiwa kumegua maneno kwenye ujumbe ndani ya nukuu za jumbe, na hivyo kufanya ionekane kana kwamba mtu alisema kitu ambacho hakukisema.

Mtafiti Oded Vanunu ameiambia BBC kwamba programu hiyo imewawezesha "watu wenye nia mbaya " kubadili mawasiliano kwenye mtandao huo.

Facebook haikutoa kauli yoyote juu ya suala hilo.

Programu hiyo ilielezewa katika mkutano wa usalama wa kimtandao unaofahamika kama Black Hat, mjini Las Vegas, kufuatia utafiti uliochapishwa na kampuni ya Checkpoint mwaka jana.

"Udhaifu wa kuingiliwa unaowaruhusu watumiaji wenye nia mbaya kubuni taarifa gushi na kufanya wizi," Ameeleza Vanunu.

Programu hii inawezesha kuingilia na kubadili nukuu za WhatsApp na kuzifanya zionekane kana kwamba mtu alikuwa ameandika kitu ambacho kiukweli hakukiandika.

"Unaweza kubadili kabisa kitu ambacho mtu anakisema ,"Alisema Bwana Vanunu." Unaweza kuharibu kabisa maneno ya nukuu ya mtu aliyoisema ."

Programu hiyo pia humruhusu mshambuliaji kubadili jinsi mtumaji wa ujumbe anavyotambulika, na hivyo kuwezesha kubadilishwa kwa chanzo cha ujumbe uchumbe na kuonekana kama ulitumwa na chanzo kingine tofauti.

Image caption WhatsApp ilifanya mabadiliko katika juhudi za kupunguza usambazaji wa taarifa potofu, kama vile kuweka ukomo wa idadi ya usamabazaji wa ujumbe

Suala la tatu lilioelezwa na watafiti limetatuliwa na Facebook. Kosa hilo linaweza kuwadanganya watumiaji kuamini kuwa walikuwa wanatuma ujumbe kwa mtu mmoja, ili hali jibu lao lilikwenda kwenye kundi la umma ambalo hawakulitarajia.

Lakini Bwana Vanunu amesema Facebook iliwaambia kuwa tatizo lingine haliwezi kutatuliwa kutokanana "ukomo wa muundo mbinu " katika WhatsApp.

Katika hasa ,mfumo wa ukusanyaji wa data unaotumiwa na WhatsApp unafanya kuwa vigumu sana kwa kampuni kufuatilia na kuthibitisha ukweli wa jumbe zinazotumwa na watumiaji.

Alipoulizwa na BBC ni kwanini timu yake ya utafiti ilitoa programu ambayo ilirahisishia watu wengine kutumia udhaifu wa hitilafu kwa watumiaji, Bwana Vanunu alitetea hatua yao, akisema alitumai itachochea mjadala.

" Whatsapp hutoa huduma kwa asilimia 30% ya wakazi wa dunia. Ni wajibu wetu.Kuna tatizo kubwa na taarifa feki na uingiliaji wa taarifa kwa lengo la kuzibadilisha. Ni muundombinu unaowahudumia watumiaji bilioni 1.5.

"Hatuwezi kuuweka kando na kusema : 'Sawa, hili halifanyiki.'"

Kusambaa kwa taarifa gushi katika WhatsApp limekuwa ni tatizo linalotia wasiwasi, hususan katika nchi kama vile India na Brazil, ambako upotoshaji wa taarifa umesababisha matukio ya ghasia na hata wakati mwingine kusababisha kifo.

WhatsApp ilifanya mabadiliko katika juhudi za kupunguza usambazaji wa taarifa potofu, kama vile kuweka ukomo wa idadi ya usamabazaji wa ujumbe.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii