Afya: 'Niligundua kuwa nimeathirika nikiwa na miaka 12'

Aloma, baba yeke Toni na mama Molly Haki miliki ya picha Toni Watson

Aloma Watson-Ratcliffe alikuwa na miaka 12 alipogundua kuwa na virusi vya Ukimwi. Sasa ana miaka 20, anaeleza ni kwa namna gani aliweza kuishi na hali hiyo alipokuwa mdogo na namna alivyojifunza kuishi kwa kuikabili hofu na unyanyapaa.

Nilipata maambukizi kutoka kwa mama yangu Molly- Nilibainika kuwa na virusi nikiwa na miaka mitatu. Hatujui kwa hakika kwa jinsi gani nilipata maambukizi, nilizaliwa kawaida bila shida, hivyo inawezekana niliambukizwa kupitia kunyonyeshwa.

Mama alifahamu kuwa ana virusi, alivipata kupitia kwa mwenzi wake alipokuwa na miaka 20, hakuwa na hali mbaya, alikuwa na afya njema naye alitaka niwe hivyohivyo.

Haki miliki ya picha Picha ya familia

Kunyonyesha ni suala la kutengeneza mahusiano mazuri kati ya mama na mtoto- ni chaguo ambalo kila mama angependa kujichagulia na ninaheshimu uchaguzi wa mama yangu. Alishauriwa na madaktari kutoninyonyesha kabisa na aliambiwa kuwa nipate dawa, lakini wazazi wangu waliona itakuwa na athari kwangu kuanza kutumia dawa za kupambana na virusi nikiwa mtoto mchanga.

Waliona ni vyema nikajengewa kinga ya asili na watoto walikuwa wakipata madhara mabaya baada ya kutumia dawa. Marafiki zangu waliopewa dawa walipata madhara kama uzio. Nina kinga yenye nguvu sana hivyo ninafikiri ulikuwa uamuzi mzuri wa wazazi wangu.

Haki miliki ya picha Aloma Watson-Ratcliffe

Tulihamia jijini Melbourne kutokea London nilipokuwa mdogo sana. Mama yangu alipitia vipindi mbalimbali vya ugonjwa - alipata nafuu kwa muda tena hali ilirejea.

Alifariki mwezi Oktoba mwaka 2001 na miezi sita baadae. Nilipokuwa na miaka mitatu, tulihamia Totnes na nikagundulika kuwa na virusi vya ukimwi.

Nilifanyiwa vipimokadhaa vya damu mara kwa mara kujua maendeleo yangu kila baada ya miezi mitatu.

Madaktari walieleza majibu kwa kutumia michoro lakini hawakuniambia jina la ugonjwa. Nilijua kulikuwa kuna jambo tofauti kunihusu.

Nilikua na ugonjwa wa namna moja nikiwa mdogo nilipata majeraha-kisha yaliondoka.

Nilikuwa na miaka 12 daktari aliponiambia nina virusi vya Ukimwi. Nakumbuka niliogopa sana na nikahisi kuwa nitakufa.

Nilisikia kuhusu virusi kwenye viwanja vya michezo, kwenye simulizi za kuchekesha kuwa virusi vilianzia kwa nyani.

Haki miliki ya picha Aloma Watson-Ratcliffe

Tayari nilikuwa na uelewa kwenye kichwa changu kuwa ni kama vile hukumu ya kifo.

Nilijawa na hofu na sikujua mtu yeyote mwenye virusi vya ukimwi, nilikuwa peke yangu na huo ulikuwa mzigo mkubwa sana.

Ilikuwa siri chungu sana ambayo sikuweza kuielewa. Nilikuwa mtoto wa kujifungia, niliyekuwa na changamoto nyingi za kijamii.

Baadhi ya wazazi walibaini kupitia kwa walimu, au wazazi wengine. Walimfikia baba yangu na kumuuliza, '' kwa nini unamuacha anakunywa maji tunayokunywa kama sisi? ''Nikimwambia rafiki, swali la kwanza angeuliza ni ''ni salama ukinywa maji ninayokunywa?'' maambukizi hayaji kwa mate lakini kwa imani hii haikunitoka kichwani mwangu.

Waalimu walikuwa wananifuata wakinihurumia walikuwa wakiniuliza, '' unaendeleaje na dawa'' na ni kama nilikuwa nawajibu '' haiwahusu!''.

Nikiwa na miaka 16 mama yangu wa kambo alisikia habari kuhusu shirika la watoto waishio na virusi vya ukimwi kupitia redio.

Kambi hiyo ilikua na watoto 100 wenye HIV na kwa siku tano ilikuwa unafundishwa kuhusu ugonjwa huo na elimu ya ngono pia unajihusisha na kufanya vitu vya kufurahisha.

Niliogopa kwenda. Sikujua kama ilikuwa inaenda kubadili maisha yangu lakini kweli ilinibadilisha. Ilikuwa ni mara ya kwanza maishani mwangu kuweza kusema ''nina virusi vya ukimwi''.Kila mtu alikuwa akisema maneno hayo, sote tulikuwa waathirika na wala haikuogopesha.

Tulizungumza kuhusu dawa na madhara yake, tuliongea kuhusu hadithi za kuchekesha, tulikuwa wenye furaha.

Ulikuwa uzoefu muhimu sana kwa sababu watu wengine wahajisikii kama wako salama- kwenye kiwanja cha michezo huwezi kujisikia salama: kwenye mahusiano hujisikii kuwa salama mpaka utakapowaambia na kufanyia kazi mapokeo yao.

Watu wengine hawajihisi kuwa salama kwenye familia zao kwa sababu ya unyanyapaa. Hivyo kuwa salama na mwenye furaha ni muhimu sana.

Haki miliki ya picha Toni Watson

Watoto na dawa za kupambana na virusi vya Ukimwi

Aloma alipatiwa dawa ya kuounguza makali ya virusi akiwa na miaka 11, mwaka mmoja kabla ya kuambiwa kuwa ameathirika.

Mtaalamu wa masuala ya ukimwi Amanda Williams anasema kumekuwa na sura inayobadilika kwenye tafiti za virusi vya ukimwi na mabadiliko makubwa kwenye dawa zinazopatikana na ushahidi kuhusu muda muafaka kuwatibu watoto.

''Kwa sababu ya majaribio tunajua madhara yake na faida za dawa kwa uwazi kabisa sasa zaidi ya miaka 20 iliyopita wakati wazazi walipokuwa hawana uhakika kuhusu madhara kama ilivyo sasa. Baadhi ya watu wana imani kali na ni vigumu kwa familia hizo kukubali dawa.

Ninafikiri watu wamepata ufahamu lakini ukosefu wa elimu kuhusu Ukimwi shuleni, elimu kuhusu ngono haitolewi, kinachoongelewa ni ugonjwa wa ukimwi kuambukizwa kwa ngono, ambapo mimi aikuupata kwa njia hiyo.

Ni vigumu wakati wote kuwaambia wenza, kuhusu maambukizi na namna ya kuwa salama. Wengi kati ya wapenzi wangu hawakuwa na shida kuhusu hali yangu tunapojadili kwa kina.

Niko na mpenzi hivi sasa na hana neno na hali yangu, ni suala la kuwa wazi na mkweli, hili linafanya kazi kwelikweli.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii