Je Meghan amemshushia umaarufu Mwanamfalme Harry?

Nigel Farage alimsifia Malkia Elizabeth na akasema anatumai ataishi miaka mingi sana Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nigel Farage alimsifia Malkia Elizabeth na akasema anatumai ataishi miaka mingi sana

Kiongozi wa chama chama kinachounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Muungano wa Ulaya Nigel Farage amewakosoa wajumbe wa familia ya ufalme wa Uingereza, akiumuelezea marehemu mama yake Malkia kama "mwenye uzito wa kupita kiasi ,mvutaji sigara na mnywaji wa vileo vikali ".

Pia amesema kuwa kiwango cha umaarufu wa mwanamfalme Harry au Duke of Sussex "kimeshuka " tangu alipokutana mkewe , Meghan.

Kiongozi huyo ametoa kauli yake alipokuwa kihudhuria kikao cha vuguvugu la mrengo wa kulia nchini Australia.

Msemaji wake amekanusha taarifa kuwa Bwana Farage alimuita Mwanamfalme Harry "Mwanamfalme anayejali ubaguzi wa rangi".

Lakini amethibitisha kuwa Bwana Farage alitoa kauli ambazo zilirekodiwa wakati wa mkutano kuhusu hatua za siasa za kihafidhinia mjini Sydney Jumamosi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan Markle

Katika rekodi ya sauti iliyolifikia gazeti la the Guardian nchini Uingereza, Bwana Farage anasikia akimsifu Malkia , akimsifia kuwa ni mtu wa "kushangaza, mwanamke wa kuigwa ".

Lakini akasema anatumai ataishi "maisha marefu, marefu sana " ili amlinde mwanamfalme wa Wales ili awe mfalme.

Inapokuja katika suala la kijana wake ,inapokuja kwa suala la mtot wa Charlie na mabadiliko ya tabia nchi , Oh maskini , oh maskini " alisema.

"Mama yake, Mstahiki Mama yake na Malkia alikuwa mneene wa mwili kidogo, mvutaji sugu wa sigara , na mnywaji wa vileo vikali aina ya gin ambaye aliishi miaka 101.

Haki miliki ya picha EPA

Kadhalika alijadili mahusiano ya Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan , akidai Umaarufu wa "kijana , shupavu , mwenye kujigamba ,mwanaume kamili " Mwanamfalme umeporomoka tangu walipokutana.

"Alikuwa Harry, kulikuwa hapa na huyu kijana mdogo, shupavu na mwenye kujivunia ujana wake, mwanaume wa kusifika, akaingia kwenye matatizo, kaanza kuoingia kwenye sherehe akivalia mavazi yasiyofaa, kunywa pombe kupihta kiasi, na kusababisha aina zote za utata,"alisema.

Halafu - afisa huyu shupavu wa Uingereza ambaye alishiriki katika jeshi la Afghanistan -akawa mtu maarufu zaidi wa kizazi cha vijana kuwahi kushuhudiwa na Ufalme kwa miaka 100.

"Halafu akakutana na Meghan Markle, na kiwango chake cha umaarufu kikashuka hadi chini."

Aliendelea kuzungumzia kauli za Mwanamfalme Harry alizotoa mwezi uliopita kwamba yeye na mkewe Meghanwanapanga kuwa na watoto zaidi ya watatu ili wawasaidie kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Bwana Farage alisema hatua hiyo "haina maana " kwasababu "idadi ya wadu duniani ni kubwa kupinduakia " katika maeneo kama vile India na Uchina.

Msemaji wake aliongeza kuwa kauli za Bwana Farage hazikutolewa kama sehemu ya hotuba yake.

"Ninachoweza kusema tu ni kwamba Charlie Boy kwa sasa ana miaka 70 na zaidi ... Namuombea Malkia aishi miaka mingi sana , Muda mrefu sana."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii