Malasia: Maajabu ya wanafunzi 'wanaopagawa'

Siti Nurannisaa Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Presentational white space

Ilikuwa asubuhi ya Ijumaa tulivu mwezi uliopita wa Julai wakati kizaazaa kilipotokea katika shule moja Kaskazini- mashariki mwa Malaysia.

Siti Nurannisaa, mwanafunzi wa miaka 17 alikuwa kati kati ya kiza zaa hicho.

Hii ni simulizi yake kuhusu kile kilichotokea.

Presentational white space

Kengele ilipolia .

Nilikuwa nimekaa kwenye dawati langu na nilikuwa nasinzia, mara nikasikia kama mtu amenigusa kwa nguvu,nimegongwa kwa nguvu kwenye mabega.

Niligeuka kuangalia ni nani aliyenigusa mara nikashtukia chumba kimekuwa giza.

Niliingiwa na uwoga.Nilihisi maumivu makali, kwenye mgongo wangu na mara baada yahapo kishwa kikaanza kunizunguka.Nikaanguka sakafunir.

Kabla sijaelewa kinachoendelea nilijipata katika 'ulimwengu mwingine'. uliyo na damu na ghasia.

Cha kuogofya zaidi niliona uso wa uovu.

Ilinisumbua sana sikuweza kutoroka. Nilifungu mdomo nikajaribu kupiga mayoe lakini sauti ilikuwa haitoki.

Nikazimia.

Presentational white space

Kelele za Siti zilisababisha taharuki shule nzima. Katika kipindi cha dakika kadhaa wanafunzi walianda kupiga mayoe madarasani mwao wakikimbia huku wengine wakilia.

Msichana mmoja alizirai baada ya kuona ''kiwili wili cheusi'' sawa na alichokiona Siti.

Presentational white space
Siti's shadow Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Presentational white space

Milango ya madarasa ya shule ya kitaifa ya upili ya Ketereh (SMK Ketereh) mjini Kelantan ilifunguka na kufungika kwa nguvu ajabu huku walimu na wanafunzi waliojawa na uwoga wakijaribu kujificha.

Waganga wa kidini kutoka jamii ya waislamu walialikwa kuja kufanya maombi ya pamoja.

Kufikia mwisho wa siku watu 39 walisadikiwa kuathiriwa na mkurupuko wa hali ya inayofahamika kama kupagawa kwa watu wengi kwa pamoja "mass hysteria".

Short presentational grey line

Kupagawa kwa watu wengi kwa pamoja "Ni majibu ya dhiki ya pamoja inayosababisha kuongezeka kwa mfumo wa neva," anasema mtaalamu wa matibabu na mwanasosholojia kutoka Marekani Robert Bartholomew.

tatizo linaloathiri mfumo wa neva mara nyingi ni vigumu kueleweka na baadhi ya wataalamu wa kimatibabu wanatibu hali hiyo kama tatizo la kiakili.

Lakini wataalamu wa magonjwa ya akili kama Dkt Simon Wessely kutoka Hospitali ya King's College mjini wanaichukulia kama "tabia ya pamoja".

"Dalili anazopata muathiriwa ni pamoja na- kuzirai, roho kudunda kwa kasi, kuumwa na kichwa, kichefu chefu, kutetemeka na kupepesuka," anasema.

"Ni tatizo ambalo mara nyingi linahusishwa na hali ya kiafya lakini halina ufafanuzi wa kiatibabu unaoelezea kinaga ubaga ni nini hasa."

Anasema mutu anaweza kupatwa na hali hiyo kutokana na ''sababu za kisaikolojia na za kijamii ".

Presentational white space
Siti Nurannisaa Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Presentational white space

Mkurupuko wake umeangaziwa mara kadhaa duniani huku baadhi ya visa vikiripotiwa kuwaathiri watu wa umri wa makamo.

Nchini Malaysia hali hiyo iliwakabili wafanyikazi wa viwandani miaka ya 1960.

Lakini siku hizi inasemekana kuwa huwaathiri watoto wa shule wakiwa kwenye mabweni yao.

Presentational white space
Msikiti Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Image caption Moja ya misikiti mingi katika mji wa Ketereh
Presentational white space

Robert Bartholomew alitumia miongo kadhaa kufanya utafiti kuhusu hali hiyo nchini Malaysia.

"Ni suala la kidini zaidi katika taifa hilo ambalo linazingatia kikamilifu muongozo wa kidini hasa miongoni mwa jamii inayoishi maeneo ya vijijini. wengi wao wanaamini nguvu za utamaduni wa jadi."

Lakini suala la hisia ya uwogo kupita kiasi ni nyeti sana. Inchi Malaysia, visa hivyo hinaawaathiri zaidi wasichana kuliko kundi lingine lolote katika jamii ya waislamu.

"Hakuna anayepinga kuwa hysteria ni hali inayowakabili wanawake zaidi," anasema Bw. Bartholomew.

Presentational white space
The Kelantan countryside Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Presentational white space

Kijiji cha Padang Lembek kinapatikana viungani mwa mji mku wa Kelantan, Kota Bharu.

Watu katika kijiji hicho kidogo wameshikamana kiasi cha kuwa kila mmoja anamjua mwenzake. Nisehemu ambaya inamkumbusha Mmalaysia yeyote jinsi jamii zao zilivyoishi kwa upendo.

Familia ya Sita inaendesha biashara ya hoteli na saluni, makaazi ambayo yamezungukwa na msikiti na mashule kadhaa.

Presentational white space
Familia ya Siti nyumbani kwao Padang Lembek Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Image caption Familia ya Siti nyumbani kwao Padang Lembek
Presentational white space

Siti na familia yake waliishi katika nyumba ya ghorofa moja, iliyotambulika kwa urahisi kutokana na rangi yake ya kijani kibichi.

Pia walikuwa na pikipki ndogo ambayo alikuwa akitumia na rafiki yake Rusydiah Roslan, ambaye anaishi hapo karibu.

"Tulikuwa tukiitumia kwenda shuleni asubuhi hiyo niliingiwa na 'mapepo'," Siti alisema.

Presentational white space
Siti Nurannisaa Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Presentational white space

Swa na msichana wengine wadogo, Siti alikumbwa na msongo wa mawazo. Anasema alihisi hali hiyo ilimtatiza zaidi katika mwaka wake wa mwisho shuleni mwaka 2018, wakati mtihani muhimu ulipokaribia.

"Nilijiandaa kwa wiki kadhaa, nikijaribu kukumbuka kile nilichosoma lakini kulikuwa na tatizo," Anasema. "Nilihisi kana kwamba hakuna kitu kinaniingia kichwani mwangu."

Kisa kilichotokea shuleni mwezi Julai kilimuacha Siti akiwa na tatizo la kupata usingizi na kukosa hamu ya kula vizuri. Ilimchukua mwezi mzima kabla ya kurejelea hali yake ya kawaida.

Short presentational grey line

Wataalamu wanasema ''mass hysteria'' mara nyingi huanza na mmtu mmoja, yaani mtu wa kwanza kujipata katika hali hiyo.

Katika kisa hiki mtu huyo ni Siti.

"Haimpati mtu kwa usiku mmoja," anasema Robert Bartholomew. "Inaanza na mtoto mmoja na baadae huwashika wengine kwa sababu ya msongo wa mawazo wanayopata kutokana na mazingira waliopo wakati huo."

Kinachohitajika ni ile hali ya taharuki inayowapata watu wengi pamoja, kwa mfano kumuona mwanafunzi mwenzako akizirai ama kupepesuka - hiyo inatosha kushtua aliyekaribu.

Presentational white space
Siti Nurannisaa Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Image caption Siti Nurannisaa
Presentational white space

Rusydiah Roslan hatawahi kusahau hali iliyokua nayo rafiki yake. "Siti alipiga kilele ya ajabu na hakuna aliyeweza kumdhibiti wakati huo,"anasema. "Hakuna aliyejua amsaidie vipi. Tuliogopa hata kumgusa."

Wasichana hao walikuwa wakipendana sana lakini tukio la mwaka uliopita hilo lillwaleta karibu zaidi. "Inatusaidia kuzungumza kuhusu kile kilichotokea," Rusydiah anasema. "Inatusaidia kusonga mbele na maisha ."

Short presentational grey line

Kutoka, SMK Ketereh inaonekana kama shule yoyote ya upili nchini Malaysia. Miti mikubwa ilitoa kivuli kizuri na kuta zake zilikuwa zimepakwa rangi nzuri ya samawati na kijani kibichi.

Makcik (shangazi) Zan alikuwa na biashara maarufu iliyojulikana na wengi kwa kuuza mchele na vyakula vinavyotokana na mapishi yake.

Alikuwa akipika chakula tukio la asubuhi ya Julai mwaka mmoja uliopita aliposikia watu wakipiga mayowe.

Presentational white space
SMK Ketereh Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Image caption SMK Ketereh, shule ya Siti Nurannisa
Presentational white space

Alipotoka nje kuangalia tatizo ni nini, aliona wasichana karibu tisa wakibebwa kutoka madarasani mwao.

Aliwafahamu baadhi yao kwa sababu ni wateja wake wa mara kwa mara. "Nilishtuka sana,"alisema.

Baadae alibuona mganga wa kienyeji akiingia shuleni na wasaidizi wake. "walichukua saa tatu humo ndani,"anakumbuka. "Nawahurumia watoto hao walichokiona siku hiyo."

Presentational white space
Local vendor Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Presentational white space

Kutoka mwezi Julai mwaka 2018 usalama wa SMK Ketereh umeimarishwa kutokana na tukio hilo.

"Uamuzi hi huo ulichukuliwa ili kuzua kisa kama hicho kisitokee tena, tumefanyia mabadiliko programu zetu na kuwabadilisha baadhi ya maafisa wetu," mmoja wa maafisa wakuu wa washule hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliiambia BBC.

Maombi ya kila siku na huduma ya ushauri nasaha pia imezinduliwa, alisema. "Usalama wa wanafunzi wetu ni jambo muhimu."

Haikubainika ushauri huo unaangazia nini hasa na ikiwa unafanywa na wataalamu wa masuala ya kiakili kwasababu afisa huyo hakuelezea zaidi ya hapo.

A map of Kelantan and its towns
Presentational white space

Wataalamu kama Robert Bartholomew wanaamini ipo haja ya kuwahamasisha wanafunzi kuhusu matukio hayo ya kupagawa hasa ikizingatiwa kuwa yamekita mizizi nchini humo.

"Wanafaa kusomeshwa kwa nini watu wengi hupagawa na hali hiyo hutokea vipi na kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine," alisema.

"Pia ni vyema kujifunza jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo na taharuki."

Maafisa wa elimu wa Malaysia hawajatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

SMK Ketereh ni moja ya shule za upili 68 mjini Kelantan lakini sio shule pekee ambayo wanafunzi wake wamekumbana na tatizo la kupagawa

Mapema mwa 2016, ilishuhudiwa katika shule kadhaa za Jimbo hilo.

Siti Ain na mama yake Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Image caption Siti Ain baada ya kumaliza shule (kulia) akiwan a mama yake ambaye anafanya biashara karibu na shule yake ya zamani
Presentational white space

Siti Ain,ambaye alisomea SMK Pengkalan Chepa 2, anasema hatawahi kuisahai shule hiyo.

"Anakumbuka jinsi alivyopagawa kwa saa kadhaa na ilivyomchukua miezi kadha kurejelea hali yake ya kawaida ," Alisema msichana huyo wa miaka 18.

Hali kama hiyo imewahi kuripotiwa katika makaazi ya watawa wa kanisa Katholiki nchini Mexico, Italia, Ufaransa na hata katika mashule ya Kosovo.

Kila kesi ni ya kivyake - Lakini hali ya kupagawa ni moja na watafiti wanasema kuwa hali hiyo huchangiwa na desturi aya kufungia watu malipamoja kwa muda mrefu chini ya uangalizi mkali.

Presentational white space
Students Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Presentational white space

Wataalamu wa saikolojia kama vile Steven Diamond, wanasema "Dalili za uchungu, uwoga na haya" ambazo mara nyingi zinahusishwa na mass hysteria"zinaashiria muathiriwa anataka watu wamhudimie kwa ukaribu".

"Wakati mwingine ni njia moja ya kueleza jinsi wanavyohisi moyoni lakini hawana uwezo wakujieleza ama hawajisikii huru kuelezea kunachowasibu" aliandika katika nakala yake moja inayohusiana na masuala ya kisaikolojia iliyochapishwa mwaka 2002.

Short presentational grey line

Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wenye shughuli nyingi kwa Siti Nurannisaa.

"Naendelea vizuri. Nimetulia nashkuru," alisema. "Sijashuhudia wala kuona kitu kibaya kwa miezi kadhaa sasa."

Alipotelea na marafiki wake wengi alipofuzu kutoka SMK Ketereh lakini hilo halijamtatiza - alimwambia mwandishi wa BBC kuwa anapendelea kuwa na marafiki wachache wa karibu.

Kwa sasa amechukua likizo ya masomo kabla ya kujiunga na Chuo.

Presentational white space
Siti Nurannisaa Haki miliki ya picha Joshua Paul for the BBC
Image caption Siti na paka wake Chomel
Presentational white space

Siku tuliokutana alinionesha kipasa sauti kidogo cha rangi nyeusi.

"Kuimba karaoke ni baadhi ya mambo ninayopenda wakati nikiwa peke yangu," anasema. Nnyimbo za Pop za muimbaji Katy Perry na nyimbo za wanamuziki wa kike wa Malaysia zinamvutia sana Siti Nurhaliza .

Presentational white space
Microphone Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Presentational white space

Kuimba kumeonesha kuwa njia bora ya kujiondolea msongo wa akili kwa msichana huyo mdogo, inamsaidia kujiamini baada ya kisa kilichompata.

"Msongo wa mawazo hufanya mwili wangu kulegea na kukosa nguvu lakini nimekuwa nikijifunza jinsi ya kukabiliana na hali hiyo," anasema. "Lengo langu ni la kuwa mtu wa kawaida na mwenye furaha."

Presentational white space
Siti na baba yake Azam Haki miliki ya picha JOSHUA PAUL FOR THE BBC
Image caption Siti na baba yake Azam Yacob, wakiwa nyumbani kwao
Presentational white space

Kufikia hapo aliuzwa unataka kuwa nini maishani?

"Afisa wa polisi wa kike alisema. "Ni mashujaa na hawaogopi lolote."

Short presentational grey line

Ripoti ya zaiada kutoka kwa Jules Rahman Ong.

Mada zinazohusiana