Tuhuma kuhusu agizo la kumpiga risasi 50 Cent 'hazina msingi'

50 Cent on stage Haki miliki ya picha Getty Images

Uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba afisa mmoja mkuu wa polisi aliwaambia maafisa wake wampige risasi 50 Cent popote watakapomuona, umekamilika.

Naibu inspekta manuel Gonzalez alishutumiwa kwa kutoa matamshi katika hafla ambayo rapa huyo maarufu Marekani jina halisi, Curtis Jackson, alitarajiwa ahudhurie.

Tuhuma hizo zilitajwa "kutokuwa na msingi" na kesi imefungwa, Luteni Thomas Antonetti ameiambia BBC Radio 1 Newsbeat.

50 Cent alisema: "Nilijua kuwa hawatofanya lolote kulihusu hili."

"Nikaacha kulizungumzia. NYPD kwa wepesi ndio gengi kali New York," aliongeza kwenye mtandao wa Instagram.

Ilidaiwa kuwa naibu Inspekta Gonzalez alitoa matamshi hayo na kujaribu kuyafanya kama mzaha, lakini aliripotiwa kwa idara ya mambo ya ndani ya NYPD.

Mwezi mmoja kabla ya tukio hilo kutuhumiwa kufanyika, afisa huyo wa polisi aliwasilisha malalamiko dhidi ya 50 cent ya kudai kunyanyaswa vikali.

Alisema rapa huyo alimtishia kwenye mtandao wa Instagram - katika kujibu tuhuma kuwa naibu inspekta Gonzalez alichunguza kwa upendeleo mojawapo ya vilabu vya burudani anayopendelea kwenda 50 Cent.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii