Akamatwa Iran licha ya kuwa na uraia wa Iran na Uingereza

Mkewe Kameel Ahmady -Shafaq Rahmani alidai kuwa maafisa wa usalama walikuja kwenye nyumba yao na " kuchukua stakabadhi, ikiwemo kadi ya kitambulisho Haki miliki ya picha FACEBOOK
Image caption Mkewe Kameel Ahmady -Shafaq Rahmani alidai kuwa maafisa wa usalama walikuja kwenye nyumba yao na " kuchukua stakabadhi, ikiwemo kadi ya kitambulisho

Mtu mwenye uraia wa nchi mbili, Uingereza na Iran amekamatwa magharibi mwa Iran, kwa mujibu wa familia yake.

Mkewe Kameel Ahmady, ambaye ni mtaalamu wa historia ya binadamu na jamii , amesma kuwa alipelekwa mahabusu Jumapili kutoka nyumbani kwake bila kuelezwa sababu.

Bwana Ahmady amefanya utafiti kuhusu ukeketaji wa wanawake pamoja na ndoa za watoto nchini Iran , miongoni mwa tafiti zingine.

Muingereza mwingine mwenye uraia wa wa nchi hizo mbili , Nazanin Zaghari-Ratcliffe, amekuwa katika mahabusu ya Iran tangu mwaka 2016 juu ya madai ya kufanya ujasusi

Mapema mwaka huu , wizara ya mambo ya nchi za nje ya Uingereza iliwashauri watu wote wenye uraia wa nchi mbili wasisafiri kwenda Iran kwasababu wako katika hatari ya kukamatwa bila kiholela.

Kukamatwa kwa hivi karibuni kwa Ahmady kunatokea huku kukiwa na hali ya wasiwasi baina ya nchi hizo , kutokana na kukamatwa kwa meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza:Uingereza kufanya kikao cha dharura kuhusu Iran

Wavuti wa wasoni ulilitaja jina la Ahmady ukimuelezea kama "Muingereza-Muiran asilia kutoka Kurdistan". Utambulisha wake wa wavuti Kitaaluma LinkedIn unasema alisomea katika vyuo vikuu vya Uingereza kikiwemo -London School of Economics na Political Science (LSE).

Msemaji wa Mtandao wa Haki za kinadamu wa Kurdistan , ulioripoti kukamatwa kwake , umesema kuwa Bwana Ahmady ameishi Iran kwa miaka mingi.

Maafisa katika nchi zote mbili bado hawajathibitisha kuwa amepelekwa mahabusu.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Bwana Ahmad amechapisha vitabu na makala kadhaa

Katika mahojiano na Idhaa ya BBC ya Kipershi BBC , mkewe Shafaq Rahmani alidai kuwa maafisa wa usalama walikuja kwenye nyumba yao na " kuchukua stakabadhi, ikiwemo kadi ya kitambulisho ".

Amesema , afisa mmoja wa mahakama katika eneo hilo baadae alithibitisha agizo la kifungo cha muda cha mwezi mmoja limetolewa dhidi ya Bwana Ahmady.

"Hawajatoa taarifa yoyote juu ya sababu ya kumkamata au hata mashtaka dhidi ya Kameel," Bi Rahmani aliandika katika Instagram.

Iran haitambui utaia wa nchi mbili na hakuna yakwimu kamili juu ya idadi ya watu waliokamatwa ambao pia wana uraia wa nchi za kigeni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii