Mgogoro wa meli ya mafuta ya Iran: Meli ya mafuta ya Iran iliokamatwa Gibraltar yaachiliwa licha ya ombi la Marekani kuizuilia

Grace 1 iliokuwa ikibeba mafuta ya Iran

Meli ya mafuta ya Iran iliokamatwa nchini Gibraltar inatarajiwa yaachiliwa mahakama ya kilele imeagiza licha ya ombi la dakika za mwisho kutoka kwa mamlaka ya Marekani.

Gibraltar ilipokea barua rasmi ya hakikisho kutoka kwa Iran kwamba meli hiyo haitapeleka mafuta yake nchini Syria

Idara ya haki nchini Marekani iliwasilisha ombi la dakika za mwisho kwa mamlaka nchini Gibraltar kuzuia kuachiliwa kwa meli hiyo ya Iran

Meli hiyo kwa jina Grace 1 iliokuwa ikibeba mafuta ilikamatwa na wanamaji wa Uingereza tarehe 4 Julai hatua iliosababisha mgogoro na Iran.

Lakini Marekani iliomba taifa hilo kufikiria tena huku kesi yake ikitarajiwa kusikilizwa saa tisa muda wa Uingereza.

Gibraltar imesema kuwa ombi hilo la Marekani linatokana na baadhi ya madai ambayo yanaangaziwa kwa sasa.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Uingereza imesema kuwa haiwezi kuzungumza kuhusu ombi hilo la Marekani.

Uingereza ilitaka meli hiyo ya Iran kuachiliwa?

Mwandshi wa maswala ya ulimwengu wa BBC Marcus Jonathan anasema kwamba Uingereza imekuwa ikitumai kwamba kuachiliwa kwa Grace 1 kutasababisha kuachiliwa kwa meli inayopeperusha bendera ya Uingereza ya Stena Impero iliokamatwa na Iran katika Ghuba.

Msemaji wa serikali ya Gibraltar pia alithibitisha kwamba uchunguzi wa polisi dhidi ya wafanyakazi wote wa nne wa meli hiyo akiwemo nahodha raia wa India umekamilika.

Mawakili wa wafanyakazi hao waliambia BBC kwamba maafisa wa polisi walisema kwamba hilo linatokana na vitendo vya serikali ya Iran na kwamba haikuwa hamu ya umma kuendelea nayo.

Meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya serikali ya Gibraltar kusema kwamba ilikuwa inaelekea Syria ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Takriban wanamaji 30 walisafirishwa kutoka Uingereza kuelekea Gibraltar ili kuwasaidia maafisa wa polisi kuizuia meli hiyo ya mafuta na mizigo yake kufuatia ombi la serikali ya Gibraltar.

Kukamatwa kwa meli hiyo kulizua mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Iran ambao umeongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Haki miliki ya picha Reuters

Hofu yatanda kati ya Iran na mataifa ya magharibi

Wiki iliopita , Uingereza ilitangaza kwamba itajiunga na jopo la Marekani la kulinda meli za kibiashara zinazosafiri kupitia njia muhimu ya meli katika mkondo wa Hormuz.

Hali ya wasiwasi kati ya Iran na magtiafa ya magharibi inatokana na mpango wa kinyuklia wa Iran.

Mwaka uliopita , Washington ilijiondoa katika mpango huo wa 2015 ili kupunguza vitendo vya kinyuklia vya Iran huku kukiwa na madai kwamba taifa hilo lilikuwa likijaribu kutengeza silaha za kinyuklia, kitu ambacho Iran imekuwa ikikana.

Tangu wakati huo hofu imetanda kati ya Iran na Marekani baada ya Washington kuimarisha vikwazo dhidi ya taifa hilo.

Uingereza na mataifa ya Ulaya yamesema kwamba bado yamesalia katika mkataba huo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii