Rais Museveni awashauri vijana waache anasa

Bwana Museveni amewashauri vijana juu ya kile alichokiita "nidhamu ya jamii" kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
Image caption Bwana Museveni amewashauri vijana juu ya kile alichokiita "nidhamu ya jamii" kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima

Rais Yoweri Museveni amewataka vijana kufuata na kulinda utamaduni wa Kiafrika na sio kudanganywa na ulimwengu wa kimagharibi ambao ameuelezea kama "unaoumwa'', limeripoti gazeti la Daily Monitor nchini humo.

"Nchi za magharibi hazina miwani ya kuona utofauti kati ya mwanamke na mwanamme . Ni wagonjwa . Urithi wa utamaduni wetu lazima udumishwe, lakini wengine utamaduni wetu unaofuatwa na 68% ya watu , ubadilishwe kwa lazima ," amesema Bwana Museveni.

Rais huyo wa Uganda ametoa kauli hizi alipokuwa akikutana na wawakilishi wa vijana kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hiyo wanaounda baraza la kitaifa la vijana- National Youth Council katika Wilaya ya Jinja Jumatano.

Bwana Museveni amewashauri vijana juu ya kile alichokiita "nidhamu ya jamii" kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na sherehe kubwa na anasa. Amesema pia anashangazwa ni pesa gani vijana wanazimwaga kwenye baa huku wakidai hawana pesa.

Image caption ''Unaenda baa unawakuta wamejaa, ukienda wanakochoma nguruwe unakuta vijana wamejaa'' amesema Museveni

"Unaenda baa unawakuta wamejaa, ukienda wanakochoma nguruwe unakuta vijana wamejaa. Huu ni utovu wa nidhamu ya jamii na ni sehemu ya tatizo tunalokabiliana nalo ," anasema Museveni.

Katika taarifa iliyotolewa na maafisa wake wa habari , Bwana Museveni alisisitizia umuhimu wa haja ya kuwa na nidhamu ya kiuchumi na akaahidi usaidizi wa serikali yake kwa vijana ambao watafungua vyama vya ushirika na kujihusisha na shughuli za uzlishaji, limeripoti gazeti la Daily Monitor.

Image caption Bwana Museveni amewashauri vijana juu ya kile alichokiita "nidhamu ya jamii" kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na sherehe kubwa na anasa

"Vijana wanapaswa kufahamu kuwa wanapozungumza na mimi, wanapozungumza na mtu ambae zamani alikuwa kijana, wakati mmoja . Nilikuwa kijana lakini kijana asiye wa kawaida, ambae alikuwa bora kuliko hata watu wazima wakati huo. Nilifundisha mabadiliko ya njia za kisasa za ukulima wakati watu wa Ankole walipokuwa wanaamini kwamba kilimo cha biashara kilikuwa ni kwa ajili ya wasomi pekee ," alisema.

Aliwashauri viongozi wa vijana kuanza wenyewe kubadilika kimawazo jambo ambalo litawasaidia kuwabadili wale walio chini ya uongozi wao .

"Hata kama itamaanisha kuwahamasisha watu kubadilika juu ya matumizi ya pesa kupitia Twitter. Ninaweza pia kutweet na nyingi ," alisema rais Museveni.

Mkutano baina ya Museveni na vijana ni moja ya misururu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya vijana.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Idadi ya wanawake wanaotumia pombe inazidi kuongezeka nchini Kenya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii