Maandamano Zimbabwe: Upinzani uliapa kukaidi marufuku ya kuandamana iliyotolewa na polisi

Nationwide demonstrations erupted in January following a crippling strike over an increase in the price of fuel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nationwide demonstrations erupted in January following a crippling strike over an increase in the price of fuel

Upinzani nchini Zimbabwe umeahirisha maandamano yaliopangwa kufanyika leo baada ya kuapa kuendelea kukaidi marufuku ya polisi dhidi ya maandamano ya kupinga serikali.

Tendai Biti kutoka chama kikuu cha upinzani nchini humo MDC ameithibitishia BBC kwamba maandamano hayo hayatofanyika kama ilivyopangwa awali.

Ameeleza kuwa uamuzi huo umeondoshwa mikononi mwao na maafisa wa polisi waliozifunga barabara zinazoelekea mjini.

Mahakama nchini humo ilitupilia mbali ombi la MDC kutaka marufuku hiyo ya polisi ifutiliwe mbali.

Mamia ya waandamanaji kadhaa waliokusanyika kukaidi marufuku hiyo, walitawanywa.

Maafisa wengi wa polisi wanapiga doria katika enoe la mjini.

Awali kundi hilo la upinzani Zimbabwe' liliapa kwamba lingeendelea kuandaa maandamano katika mji mkuu Harare na kukaidi marufuku ya polisi.

Chama cha MDC kiliitisha maandamano hayo ya umma kulalamika namna serikali inavyoshughulikia uchumi wa nchi.

Takriban raia milioni tano wa Zimbabwe wanahitaji msaada kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maandamano ya umma yalifanyika mjini Harare kushinikiza rais Robert Mugabe ajiuzulu mnamo 2017

MDC kimesema kimewahakikishia maafisa wa utawala kwamba maandamano hayo yangekuwa ya amani.

Hatahivyo, polisi wamesema wana ushahidi kwamba maandamano hayo yaliopangwa yangekumbwa na ghasia.

"Ilani ya zuio" inayopiga marufuku maandamano hayo imetolewa na maafisa mjini Harare, alisema msemaji wa polisi Paul Nyathi.

Katika kuijibu kauli hiyo, afisa wa MDC aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba chama hicho hakifahamu kuhusu zuio lolote na kwamba maandamano yataendelea kama yalivyopangwa.

"Maisha nchini Zimbabwe leo ni mabaya kuliko yalivyokuwa chini ya utawala wa Robert Mugabe," mwanasiasa wa MDC Fadzayi Mahere ameiambia BBC.

Polisi walitawanywa hadi katika makao makuu ya chama cha MDC na watu wamelisusia eneo la mjini huku maduka yakiwa yamefungwa kinyume n ailivyo kawaida anaeleza mwandishi wa BBC Shingai Nyoka mjini Harare.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Afisa wa jeshi la taifa Zimbabwe (ZNA) akishika doria

Haya yote yanajiri baada ya takriban wafuasi wasita wa mashirika ya kiraia na wa upinzani kudaiwa kutekwa na kuteswa mapema wiki hii.

Shirika la kutetea haki za binaadamu Zimbabwe linasema waathiriwa walituhumiwa kushinikiza watu kuandamana.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanaituhumu serikali kwa kutoweka kwa watu hao lakini maafisa wa serikali wamekana kuhusika.

Uingereza na Marekani zimeelezea wasiwasi kuhusu ripoti hizo.

Hali imefikaje hapa?

Katika miezi ya hivi karibuni uchumi wa Zimbabwe umetiririka, na kuongezea malalamiko yaliopo tayari dhidi ya chama tawala Zanu PF kilicho chini ya ya utawala wa Rais Emmerson Mnangagwa.

Mnangagwa aliingia madarakani mnamo NOvemba 2017 baada ya kiongozi mkongwe na wa muda mrefu kutimuliwa katika mapinduzi ya kijeshi.

Aliitisha uchaguzi, uliofanyika mwaka uliofuata Julai 30 ambapo alishnda.

Katika kampeni kuelekea kuchaguliwa kwake aliahidi mageuzi ya kidemokrasia na kuufufua uchumi wa nchi baada ya kudorora kwa miaka kadhaa chini ya utawala wa Mugabe.

Lakini matumaini yaliokuwepo na mabadiliko yalioshuhudiwa baada ya kutimuliwa Mugabe yamefifia wakati uchumi wa nchi unayoyoma.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Emmerson Mnangagwa anajaribu kuufufua uchumi unaodorora Zimbabwe

Makundi ya upinzani yanahisi kuwa rais ameshindwa kutimiza ahadi alizotoa baada ya kuchaguliwa kwake katika uchaguzi uliokumbwa na mzozo.

Kumekuwa na hofu hatahivyo, kwamba maandamano mengine Harare na katika miji mingine mikubwa huenda yakachangia kuidhinishwa misako sawana ilioshuhuidwa mnamo Januari.

Katika maandamano hayo, takriban watu 12 waliuawa na wengine wengi walipigwa na maafisa wa usalama , makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini humo yanasema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC