Apunguza kilo 89 bila kufanyiwa upasuaji wa kimatibabu
Huwezi kusikiliza tena

Apunguza kilo 89 bila kufanyiwa upasuaji

Jason Anderson alikua anaugua maradhi ya shinikizo la damu, kisukati na tatizo la kulala.

Madaktari walitaka kumfanyia upasuaji wa dharura wa kupunguza uzani mtu huyo mkaazi wa Nuneaton nchini Uingereza baada ya kumfanyia uchunguzi wa kimatibabu.

Lakini alikataa na kusema atapunguza uzani mwenyewe bila kufanyiwa upasuaji.

Alifanikiwa kupunguza kilo 89 katika kipindi cha miaka miwili hali iliosaidia afya yake kuimarika.