Eduard Pernkopf: Kitabu cha Wanazi bado kinatumiwa kufanya upasuaji

Mchoro unaoonesha sehemu ya uso wa mwanamume uliofanyiwa upasuaji Haki miliki ya picha Erich Lepier
Image caption Mchoro unaoonesha sehemu ya uso wa mwanamume uliofanyiwa upasuaji

Mtaalamu wa upasuaji wa neva Dkt Susan Mackinnon alipohitaji usaidizi wakati wa upasuaji alitumia kitabu kilichoandikwa karne ya 20 kinachoelezea mfumo wa mwili wa binadamu.

Kwa kutumia Michoro migumu iliyo kwenye kitabu hicho iliyochorwa kwa mikono -Dkt Mackinnon, kutoka Chuo Kikuu cha Washington mjini St Louis, aliweza kukamilisha upasauaji wa mwili wa binadamu.

Kitabu hicho kinachofahamika kama Pernkopf Topographic Anatomy of Man, kinatajwa kuwa mfano mzuri wa michoro ya mwili wa binadamu duniani.

Hadi wa leo kitabu hicho kinasifika kwa jinsi mwandishi alivyoelezea kwa undani kuhusu mwili wa binadamu kwa kutumia michoro ya kupendeza kuliko kitabu kingine chochote.

Ngozi, misuli, mishipa, viungo na mfupaya binadamu katika kitabu hicho imefunuliwa kwa undani wa picha, bila shaka mtu mwenye moyo dhaifu hawezi kukisoma.

Lakini kitabu hicho kinachojulikana kama ramani ya mwili wabinadamu (Pernkopf's Atlas) hakichapishwi tena- japo kuna matoleo kadhaa ambayo - yanawezwa kuuzwa mitandaoni kwa maelfu ya pauni.

Haki miliki ya picha Keiligh Baker
Image caption Nakala kadhaa ya ramani ya Pernkopf zimehifadhiwa katika maktaba nchini Uingereza

Hii ni kwa sababu ufanisi wa kitabu hicho umetokana na miili ya mamia ya wanadamu waliouawa kwa kukatwa katwa na Wanazi - ambayo inaoneshwa katika maelfu ya kurasa za kitabu hicho.

Wakosoaji wanasema kitabu hicho kimetengwa na zama za Adolf Hitler na wanasayansi wanakabiliwa na wakati mgumu kujitenga maadili yanayohusika katika matumizi yake.

Dkt Mackinnon anasema asili ya kitabu hicho haimfurahishi, lakini anakitumia kwa sababu ni sehemu muhimu ya "daktari wa upasuaji" - na kwamba hakuweza kufanya kazi yake bila kuwa nacho

Rabbi Joseph Polak - manusura wa mauaji na profesa wa sheria za afya - anaamini kitabu hicho ukizingatia maadili ni "ni kibaya" kwa sababu kimetokana na "uovu halisi, lakini kinaweza kutumika kutoa huduma njema".

Kitabu hicho ni mradi wa miaka 20 wa daktari mashuhuri wa Wanazi Eduard Pernkopf, ambaye alipanda daraja tofauti za kiamasomo nchini Austria kutokana na ushirikiano wake wa karibu na chama Adolf Hitler.

Wafanyikazi wenzake walimtaja kama mfuasi "sugu" wa chama cha Kisosholisti, kutoka mwaka 1938, na alivalia sare za Nazi kwenda kazini kila siku.

Haki miliki ya picha None
Image caption Pernkopf na washirika wake

Alipopandishwa daraja na kuwa mkuu wa kitengo cha afya katika Chuo Kikuu cha Vienna, aliwafuta kazi wayahudi wote katika kitengo hich, ikiwa ni pamoja na washindi watatu wa Tuzo ya Nobel .

Mwaka 1939, sheria mpya yautawala wa Hitler, ilihitaji miili ya wafungwa wote waliouawa ipelekwe mara moja katika kitengo cha elimu ya mwili wa binadamu kwa ajili ya kufanyia utafiti na masomo.

Wakati huo Pernkopf alifanya kazi saa 18 kwa siku kupasua miili ya maiti, huku kundi la wasanii wa uchoraji wakichora sehemuza miili hiyo kwa kitabu chake.

Wakati mwingine taasisi hiyo ilijaa miili ya watu hadi mauaji yakasitishwa.

Dkt Sabine Hildebrandt,kutoka Chuo Kiku cha Harvard kitengo cha matibabu, anasema karibu michoro 800 katika kitabu hicho ni ya miili ya wafungwa wa kisiasa.

Inajumuisha wanaume na wanawake walioshiriki mapenzi ya jinsia moja, wapinzani wa kisiasa na wayahudi.

Katika toleo la kwanza la kitabu hicho, iliochapishwa mwaka 1937, saini inayoonesha maelezo ya Erich Lepier na Karl Endtresser ilijumuisha swastikas na taa maalum ya insignia ya SS.

Hata katika toleo la pili la mwaka 1964 iliyochapishwa lugha ya Kiingereza saini hiyo ilijumuisha ishara ya Hitler lakini ishara hiyo ya Wanazi ilitolewa katika nakala zilizofuata za kitabu hicho.

Haki miliki ya picha Erich Lepier
Image caption Saini ya Erich Lepier ilijumuishwa kwenye swastika

Maelfu ya nakala za ramani iliuzwa kote duniani, na ilitafsiriwa kwa kutumia lugha tano. Mwanzo wa ramani hizo zilijumuishwa kwenye vitabu kwa kutumia "michoro ya ya kipekee na ya kuvutia" huku ikiepuka kutaja maovuyaliopita .

Ni hadi miaka ya 1990 ambapo wanafunzi na wasomi walianza kuhoji watu waliokuwa kwenye ramani hizo ni kina nani na baada ya historia ya ukatili wao kufichuliwa ramani hizo ziliacha kuchapishwa mwaka 1994.

Wapasuaji wa Taasisi ya upasuaji ya Royal College wanasema ramani hizo hazitumiki nchini Uingereza, lakini zimehifadhiwa katika maktaba kama sehemu kumbu kumbu ya historia.

Hata hivyo utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalamu wa upasuaji wa ubongo na wale wa upasuajiwa neva waligundua 59% ramani za Pernkopf zinatumika kwa 13% kwa sasa.

69% ya wale walioshiriki utafiti huo walisema hawaoni tatizo kuzitumia ramani hiyo ali mradi wanafahamu historia yake, 15% hakusihisi vizuri kuzitumia na 17% hawakufanya uamuzi kuhusu suala hilo.

Dkt Mackinnon anasema hakuna kitu "kinaweza kufananishwa" uhalisia wa kitabu hicho na maelezo yake, hususan utumizi wake katika upasuaji mgumu kwa sababu unamsaidia sana" kinasaidia kutoa maelekezo yanayosaidia kufikia mishipa midogo ambayo inamfanya mtu kuhisi uchungu".

Lakini anasema kuwa anahakikisha kila mtu anaetumia kitabu hicho kwa upasuaji anaelewa chimbuko lake.

"Nilipogundua historia mbaya ya ramani hiyo nilianza kukiweka mbali na meza yangu ya upasuaji," anasema.

Haki miliki ya picha Washington University/ St. Louis
Image caption Dkt Susan Mackinnon

Mwaka jana, Rabbi Polak na mwanahistoria wa matibabu na ambaye pia ni mtaalamu wa magonjwa ya akili Profesa Michael Grodin, aliandaa warsha ya kutoa (majibu ya kitaalamu kwa kuzingatia maadili ya Kiyahudi ya matibabua) ikiwa ni sawa kutumia ramani hiyo ya upasuaji kama kwa kuzingatia Uzoefu wa Dkt Mackinnon.

Walihitimisha kuwa viongozi wengi wa Kiyahudi wangeruhusu utumiaji wa picha hizo kuokoa maisha ya watu - chini ya masharti historia ya ukatil ilijulishwa, kwa hivyo wahasiriwa walipewa baadhi ya hadhi wanayodaiwa.

Rabbi Polak, aliimbia BBC: "Angalia mfano wa Dkt Mackinnon - hakuweza kujua neva iko wapi wakati licha ya uzoefu wake katika nyanja ya upasuaji. Mgonjwa alimwambia 'Naomba unikate mguu ikiwa huwezi kupata mshipa huo haupatikani' - hakuna mtu angelitaka kujipata katika hali kama hiyo.

"Kwa hivyo hakuwa na budi kupendekeza kitabu cha Pernkopf kilicho na ramani ya upasuaji kutumika kwa sababu kilimsaidia kufikia mfumo wa neva kutokana na michoro hii.

"Aliniuliza, kama mtafakari wa maadili, juu ya hali hiyo. Nami nikamwambia, ikiwa hii itamponya mtu huyu na kuwapa maisha yao, basi hakuna shaka kwamba aturu inaweza kutumika."

Haki miliki ya picha Washington University/ St. Louis
Image caption Dkt Mackinnon wakati wa upasuaji

Pernkopf alikamatwa baada ya vita na kufutwa atkika Chuo Kikuu. Alizuiliwa jela ya kambi ya vita kwa miaka mitatu lakini hakufunguliwa mashtaka ya uhalifu.

Baada ya kuachiliwa huru alirejea Chuo Kikuu na kuendelea kufanyia kazi kitabu chake na kuchapisha toleo la tatu mwaka 1952.

Alifariki dunia mwaka 1955, muda mfupi kabla ya kuchapishwa kwa toleo la nne la kitabu hicho kilicho na ramani ya upasuaji.

Zaidi ya miaka 60 baadae, kitabu hicho bado ni moja ya vitabu muhimu kilicho na maelezo na michoro ya kina kuhusu masuala ya upasuaji, kwa mujibu wa Dkt Hildebrandt, ambaye anafundisha sayansi ya mwili wa binadamu.

"Badhi yetu tumezoea 'kuona' tunakitumia wakati tunapokuw ana swali. Ukweli ni kwamba wapusuaji wa mishipa ya neva wanakiona kizuri sana kutokana na maelezo yake ya kina," alisema.

Lakini anaongeza kuwa: "Mimi binafsi situmii michoro ya Pernkopf ninapofunza somo la anatomia hadi nie na muda wa kuzungumzia historia ya kitabu hicho."

Haki miliki ya picha Dr Sabine Hildebrandt
Image caption Dkt Sabine Hildebrandt ameandika kwa kina kuhusu kitabu hicho cha ramani ya upasuaji

Dkt Jonathan Ives, mtaalam wa masuala ya akili kutoka Chuo Kikuu cha Bristol, anakubaliana kwamba "ramani hiyo ni" ya kushangaza "lakini anasema imechanganywa na" zamani zake za kutisha".

"Ikiwa tunafaidika kielimu kutokana na maelezo yake inamaanisha tunaunga mkono zama za kutisha ya Adolf Hitler," anasema.

"Japo tuanaweza tukihoji tusipokitumia kitabu hicho huenda kikapotea huenda kikatumika kuwakumbusha watu maovu yaliopita."

Kwa Dkt Mackinnon, kinasalia kuwa kiungo muhimu- hata mambo ya kale hayawezi kusahaulika.

"Ningefikiria kuwa kama daktari anayefuata maadili ningechukichulia kama vile nilipaswa kutumia rasilimali yoyote ya kielimu ambayo nafikiri itanisaidia kuongeza ujuzi," anasema, na kuongeza kwamba mgonjwa wake anatarajia hilo kutoka kwake.

Mada zinazohusiana