Masomo chini ya miti changamoto kwa Waganda

Wanafunzi katika shule ya msingi ya Bukedea, karibu na mji wa Mbale, mashariki mwa Uganda, wakiendelea na masomo chini ya mti
Image caption Wanafunzi katika shule ya msingi ya Bukedea, karibu na mji wa Mbale, mashariki mwa Uganda, wakiendelea na masomo chini ya mti

Katika mataifa mengi ya Afrika, yakiwemo yale ya Afrika Mashariki, viongozi wamekuwa wakitangaza kuwa nchi serikali zinao zinatoa elimu bure katika shule za umma. Hata hivyo miundo mbinu ya elimu ya bure imekuwa ni changamoto kubwa ya utoaji wa elimu kwa baadhi ya maeneo ya nchi hizo.

Baadhi ya shule zimekuwa na ukosefu wa miundombinu na baadhi ya ile iliyopo iko katika hali duni inayofanya mchakato mzima wa ufundishaji na masomo katika shule za umma kuwa mgumu.

Shule ya Msingi ya Kachage, ni moja ya mifano ya shule ambazo zinakabiliwa na changamoto kubwa ya miundo mbinu.

Ikipatikana wilayani Bukedea, karibu na mji wa Mbale, mashariki mwa Uganda, Shule hii ina madarasa manne pekee.

Wanafunzi wa madarasa mengine wanalazimika kusomea chini ya miti iliyotapakaa katika uwanja wa shule hiyo, alibaini mwandishi wa BBC Roncliff Odit alipokuwa Uganda hivi karibuni.

Image caption Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Bukedea Okurut Levy (pichani mbele ya wanafunzi ) anasema imekuwa ni changamoto kubwa kuwafundisha watoto kando ya barabara

Licha ya kwamba shule hii ilianzishwa mwaka 2012, miaka saba 7 baadae bado imesalia na madarasa manne tu.

Kutokana na kwamba shule ya Kachage ipo kando ya barabara kuu ya kutoka Mbale kuelekea mjini Soroti, kila mara masomo hutatizwa na kelele za malori na magari mengine ya kusafirisha mizigo na abiria.

Walimu wa shule hiyo wanasema masomo yanatatizwa kila mara na jua kali, na vumbi jingi.

''Hawa watoto wetu tunaowafundisha wanakaa chini kwenye vumbi, hawana hata madawati, wanaweka vitabu vyao chini, hawaweza hata kuandika vizuri, kwasababu ukiweka daftari lako chini au kwenye mguu wako hauwezi kuandika vizuri, hii pia ni shida yetu'', alisema.

Hapa sisi tunafundishia kando na barabara, kama gari kubwa inapita kama hii, watoto hawawezi kusikia maneno tunayowaambia, mawazo yao yote yanaelekea barabarani. Sasa sisi tunachoiomba serikali itusaidie itujengee madarasa'' alisema Mwalimu mkuu wa shule Kachage Okurut Levy huku lori likipita nyuma yake kando ya uwanja unaotumiwa kama darasa.

Image caption Shule ya msingi Ugamba iliyopo mkoani Tabora Tanzania pia iliripotiwa kuwa na uhaba wa madarasa ya kusomea

''Hapa watoto wetu wanakaa chini, mvua ikinyesha, sare zao za shule zinachafuka, hata wanaweza kupata magonjwa kwasababu wanakaa mahala pachafu kabisa'', asisistiza Mwalimu Mkuu.

Lakini licha ya hali hiyo ngumu, bado wanafunzi wa shule ya msingi ya Kachage walijitahidi wakati wa mtihani wa kitaifa mwaka uliopita.

Saa walimu na wakuu wa shule hiyo wanatoa mwito kwa serikali kuu na wahisani kuingilia kati ili kusuluhisha tatizo hilo.

Image caption Wanafunzi katika moja ya madarasa ya shule ya msingi ya umma nchini Kenya

Si mara ya kwanza kusikia taarifa za wanafunzi wanaosomea nje au chini ya mti.

Katika nchi jirani ya Tanzania shule ya msingi Ugamba iliyopo mkoani Tabora, wanafunzi waliripotiwa kusoma nje.

Uhaba wa madarasa bado ni changamoto kwa baadhi shule nchini Tanzania.

Katika nchi jirani ya Kenya pia hali si tofauti, baadhi ya shule za umma zimekuwa zikikabiliwa na uhaba wa miundo mbinu hususan katika maeneo ya vijijini ambapo watoto wa shule wamekuwa walikabiliwa na ukosefu wa madawati na uhaba wa vitabu.

Ripoti ya hali ya elimu Barani Afrika iliyotolewa na Benki ya dunia mwezi Februari mwaka 2019, iliziorodhesha nchi za Uganda na Tanzania katika kundi la pili la mataifa yenye kiwango cha juu cha watoto wanaoachia katikati masomo ya shule ya msingi. Baadhi ya sababu zilizochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika mataifa hayo ni pamoja na kutokuwepo kwa shule karibu na maeneo ya vijijini. Kuongeza idadi ya madarasa katika shule za msingi zilizopo

Ripoti hiyo pia ilipendekeza Kuhakikisha shule zinatenga sehemu za kujisaidia kwa watoto wa kiume na wakike. Ukosefu wa vyoo na maji umetajwa kuwa chanzo cha wasichana kugoma kuenda shuleniKutumia teknolojia ya kisasa kuimarisha mafunzo na mifumo wa elimu.

Wachanganuzi wa masuala ya elimu wamekuwa wakizikosoa serikali za mataifa ya Afrika kwa kutoa ahadi za utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za umma huku shule hizo zikikabiliwa na uhaba wa miundo mbili kama vile madawati, vitabu na madarasa havipo vya kutosha

Unaweza pia kusikiliza hii :

.

Huwezi kusikiliza tena
Mpango wa elimu bila malipo Tanzania umefanikiwa?

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii