Akina dada wa Khachaturyan ambao walimuua baba yao wavutia nyoyo za raia wa Urusi

Madada wa Khachaturyantarehe 26 Juni 19 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakati wa mauaji ya baba yao , Angelina (kushoto) alikuwa 18, Maria (katikati) alikuwa na umri wa miaka 17 na Krestina 19

Mwezi Julai 2018 akina dada watatu wenyeumri mdogo walimdunga visu na kumpiga baba yao hadi kufa akiwa usingizini , katika nyumba yao iliopo mjini Moscow.

Wachunguzi wamethibitisha kwamba baba yao aliwadhulumu kimwili na kimawazo kwa miaka kadhaa.

Wakishtakiwa kwa mauaji , dada hao na kile ambacho kitafanyika baadaye ndio limekuwa swala kuu la mjadala nchini Urusi uliotiwa saini na takriban watu 300,000 wakiwasilisha ombi la kutaka waachiliwe huru.

Ni nini kilichomfanyikia baba yao?

Usiku wa tarehe 27 Julai 2018 Mikhail Khachaturyan, 57, aliwaita wanawe Krestina, Angelina na Maria, ambaye alikuwa mtoto mdogo wakati huo mmoja baada ya mmoja katika chumba chake.

Aliwakemea kwa kutoosha nyumba yao vizuri na kuwapulizia gesi ilio na pilipili usoni mwao.

Baadaye alipokuwa amelala wasichana hao walimshambulia kwa kisu , nyundo na gesi hiyo ya pilipili na kumjeruhi vibaya kichwani, shingoni na kifuani.

Alipatikana na zaidi ya majeraha 30 ya kisu. Wasichana hao baadaye waliwaita maafisa wa polisi na wakakamatwa katika eneo la tukio.

Uchunguzi uliofanywa ulifichua historia ya muda mrefu ya mgogoro wa nyumbani.

Khachaturyan alikua akiwapiga wanawe mara kwa mara kwa kipindi cha miaka mitatu , akiwatesa kuwafanya kama wafungwa mbali na kuwanyanyasa kijinsia.

Ushahidi huo dhidi ya baba yao upo katika kesi yao.

Tuangazie mgogoro wa kinyumbani

Kesi hiyo ilibadilika na kuwa mjadala mkubwa nchini Urusi .

Makundi ya haki za kibinadamu yalihoji kwamba madada hao sio wahalifu lakini walikuwa waathiriwa , kwa kuwa hawakuwa na njia za kupata usaidizi na ulinzi kutoka kwa baba yao.

Hatahivyo hakuna sheria inayowalinda waathiriwa wa migogoro ya nyumbani nchini Urusi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wengi walifanya maandamano wakitaka madada hao kuachiliwa huru.

Chini ya mabadiliko ya kisheria yalioanzishwa 2017, mshtakiwa anayempiga mmoja wa wanafamilia lakini sio vibaya sana wa kulazwa hospitali atapigwa faini ama hata kufungwa kwa wiki mbili.

Maafisa wa polisi nchini Urusi wanalichukulia swala la mgogoro nyumbani kama swala la kifamilia na kutoa msaada mdogo ama bila usaidizi wowote ule.

Mama ya dada hao ambaye pia alikuwa akipigwa na kudhulumiwa na mumewe katika siku za nyuma aliripoti unyanyasaji huo kwa polisi .

Majirani wa familia hiyo ambao walikuwa wakimuogopa sana bwana Khachaturyan pia hawakusakwa kumripoti kwa polisi.

Lakini hakuna ushahidi kwamba maafisa wa polisi walichukua hatua zozote kufuatia malalamishi hayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mama ya wasichana hao Aurelia Dunduk anasema kwmba mumewe alimfukuza kutoka nyumba hiyo 2015

Wakati wa mauaji hayo mama ya watoto hao alikuwa haishi nao na Khachaturyan alikuwa amewakataza watoto wake kuwasiliana naye.

Kulingana na wataalam wa akili, wasichana hao waliishi kwa kujitenga na kwamba walikuwa wakiugua shinikizo la akili.

Je ni nini kilichotokea wakati wa uchunguzi?

Kesi ya akina dada hao wa Khachaturyan imekuwa ikiendelea polepole.

Hawako tena kizuizini, lakini wamewekewa masharti: Hawawezi kuzungumza na waandishi habari ama wenyewe kwa wenyewe.

Waendesha mashtaka wanasisitiza kuwa mauaji ya Khachaturyan yalipangwa, alipokuwa amelala madada hao walipanga vitendo vyao , baada ya kuchukua na kukificha kisu mapema asubuhi.

Lengo lao lilikuwa kulipa kisasi, wanahoji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Akina dada hao (Angelina kwenye picha) alihudhuria kesi mwezi Juni 2019

Iwapo watapatikana na hatia chini ya shtaka hilo akina dada hao watakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.

Inadaiwa kuwa Angelina alichukua nyundo, Maria akashika kisu na Kristina pilipili hiyo ya kupulizia machoni.

Hatahivyo , wakili wa madada hao wanasema kwamba mauaji hayo yalikuwa kitendo cha kujilinda.

Sheria dhidi ya uhalifu nchini Urusi inaruhusu kujilinda sio tu katika kesi za uchokozi wa moja kwa moja lakini pia katika kesi mbaya za uhalifu kama vile utekaji nyara ambapo mwathiriwa anateswa.

Mawakili wa wasichana hao wanasema kwamba wateja wao walikuwa waathiriwa wa uhalifu uliokuwa ukiendelea na kwamba wanapaswa kuachiliwa.

Mawakili hao wanatumai kwamba kesi hiyo itatupiliwa mbali baada ya uchunguzi kubaini kwamba baba yao alikua akiwatesa kuanzia mwaka 2014.

Mashirika ya haki za kibinadamu na raia wengi wa Urusi sasa yanataka sheria kubadilishwa na mikakati kutolewa kama vile nyumba za serikali zinazofadhiliwa, kutoa maagizo ya kuzuia mbali na kutoa mafunzo ya kubadili tabia.

Je migogoro ya nyumbani imeenea kwa kiwango gani?

Hakuna data kuhusu jinsi wanawake wengi wanavyoathirika kutoka kwa ghasia nchini Urusi , ni makadirio pekee , lakini kulingana na makundi ya haki za kibinadamu inaweza kuhusisha mtu mmoja katika kila familia.

Baadhi ya visa vingine vya kushangaza ambavyo vimegonga vichwa vya habari , ni pamoja na kile kisa cha Margarita Gracheva, ambaye mumewe alimkata mikono yake kwa kutumia shoka kutokamna na wivu.

Baadhi ya wataalam wanasema kwamba asilimia 80 ya wanawake wanaoshikiliwa katika magereza nchini Urusi kwa mauaji walimuua mshambuliaji katika mgogoro wa kinyumbani wakijilinda.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii