Shinikizo kubwa la damu kwa wenye umri wa miaka 30- 40 kunaweza kusababisha madhara ya afya ya ubongo

Woman working with child Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wenye umri wa miaka 30 mara nyingi huwa wana majukumu mengi ya familia na kazi

Watu wenye umri wa kati ya miaka 30 wanahitaji kuwa makini na shinikizo la damu ili kujilinda na afya ya ubongo katika maisha yao ya baadaye, utafiti unasema

Kuna namna ya kulinda afya hiyo ya ubongo mpaka mtu anapofika mwanzoni mwa miaka 50.

Utafiti wa watu 500 ambao walizaliwa mwaka 1946, uliangalia jinsi shinikizo la damu linaweza kuleta madhara katika mishipa ya damu na ubongo .

Wataalamu wanasema kupanda kwa mapigo ya moyo ni jambo linaweza kuwasumbua watu wenye umri kati ya miaka 30 mpaka 40 na kuhusisha madhara kwenye ubongo.

Hii sio mara ya kwanza kuhusisha shinikizo la damu na umri wa watu wa katikati ambao wako kweny hatari zaidi, wanasayansi bado wanataka kuelewa zaidi kuhusu lini na namna hali hiyo inaweza kutokea.

Kuongezeka kwa tatizo la shinikizo la damu kati ya umri wa miaka 36 na 43 yanahusha na kusinyaa kwa ubongo.

"Ubongo wa kila mtu unaweza kupata uharibifu kidogo kadri muda unavyoenda , lakini hali hiyo huwakumba zaidi wale walio na shida ya afya ya akili.

Na vilevile wakati utafiti huu ukifanyika haukuonyesha dalili za watu ambao wana matatizo ya kumbukumbu" ,

mtafiti anasema - hivyo wataendelea kufuatilia kwa karibu na kufanya utafiti zaidi kujua dalili zake.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ongezeko la matatizo ya shinikizo la damu kati ya miaka 43 na 53 lilihusishwa pia na dalilli za mishipa ya damu au kupooza kwa upande mmoja kwa watu wanapofika umri wa miaka 70.

Profesa Jonathan Schott aliyeongoza utafiti huo anasema shinikizo la damu katika umri wa miaka 30 kunaweza kuleta madhara katika afya ya akili kwa miongo minne ijayo.

Ufuatiliaji na utatuzi unalenga kuboresha afya ya ubongo kwa kuwalenga watu walio katika umri wa miaka 30.

Profesa Schott aliiambia BBC kuwa kwa sasa watu wenye umri wa miaka ya 40 wako kwenye hatari kwa asilimia 50. Takwimu yao imependekeza kuwa matatizo ya shinikizo la damu yanapaswa kutambuliwa mapema.

Paul Leeson, Profesa kutoka chuo kikuu cha Oxford, alisema: "Kwa muda tunafahamu kuwa kuna watu ambao wana shinikizo la damu la mapigo ya moyo kupanda baadae wanapata matatizo ya kiafya katika ubongo.

"Kile ambacho madaktari wamekuwa wakibishana ni namna ya kutibu shinikizo la damu kwa vijana na kuzuia mabadiliko kutokea katika ubongo".

"Njia mbadala ni kile ambacho wanaona ni sawa kukifanyia kazi kwa sasa, lakini pia ni kusubiri mpaka hapo baadae watakapoanza kuangalia shinikizo la damu kuwa ni ugonjwa hatari kwa sababu tunajua sasa kuwa mabadiliko mengi yanayoweza kutokea katika ubongo, chanzo ni shinikizo la damu".

Matokeo ya utafiti huu yanaunga mkono wazo kwamba kunaweza kuwa na vipindi muhimu maishani, kama vile katika miaka ya 30 na 40, shinikizo la damu linaongeza kasi ya uharibifu ndani ya ubongo.

Utafiti tayari unashauri kwamba matibabu ya haraka zaidi ya shinikizo la damu katika miaka ya hivi karibuni yanaweza kuboresha afya ya ubongo ya vizazi vya zamani vya leo.

"Lazima tuendelee kuwaelimisha kujua namna ya kudhibiti shinikizo la damu hata kwa wale walio katika umri mdogo."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii