Mmarekani mweusi ahamia Ghana 'kutoroka ubaguzi wa rangi'

Obadele Kambon na familia yake Haki miliki ya picha Obadele Kambon
Image caption Msoi Obadele Kambon anaishi Ghana na familia yake

Obadele Kambon, Mmarekani mwenye asili ya kiafrika hajawahi kujutia hatua yake ya kuhamia nchini Ghana tangu mwaka 2008.

Aliapa kutorejea tena nchini humo baada ya tukio la kukamatwa kwake analoamini lilichochewa na ubaguzi wa rangi.

Bw Kambon ambaye sasa ameanza upya maisha katika taifa ambalo lilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa anasema kuwa anafurahia uhuru aliokosa nchini Marekani alikozaliwa.

Anasema hana hofu ya kukamatwa na polisi au cha kuogofya zaidi kuuawa kwa mwanawe wa kiume.

Hiyo ni hali iliyomkumba Tamara Rice aliyekuwa na miaka 12 ambaye aliuawa katika bustani ya Cleveland, Ohio, mwaka 2014 akiwa anacheza na bunduki badia ambayo polisi walidhani ya kweli.

Kukamatwa kimakosa

Kifo cha mvulana huyo mdogo kilisababisha maandamano makubwa mjini Cleveland, na kuwa mwanzo wa vugu vugu la kupigania uhuru wa tu weusi maarufu ''Black Lives Matter''.

Bw. Kambon anasema mwamko mpya maishani mwake ulikuwa mwaka 2007 alipokamatwa na kushtakiwa mjini Chicago - alipokuwa anaishi - baada ya kutuhumi wa na maafisa wa polisi kwa kuweka bunduki chini ya kiti cha gari lake kwa lengo la kuitumia kuwajeruhi watu.

Anakumbuka kesi hiyo hicho kwa mshtuko mkubwa na wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yake, aliapa: "Kutokaribia maeneo yanayolindwa na maafisa wa polisi wazungu asije akafungwa na kutenganishwa na familia, mke na mtoto wake kufumba macho na kufumbua."

Bw Kambon - ambaye ali dola 30,000 (£24,000) na kuhamia mji mkuu wa Ghana, Accra, mwaka uliofuata.

Mke wake, Kala aliungana nae na wanandoa hao wana watoto watatu- Ama, Kwaku na Akosua.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kasri la watumwa katika pwani ya Ghana sasa ni kivutio kikubw acha watalii

Alijiingiza katika Imani ya Kiafrika

Bw. Kambon alianza kusomea shahada ya uzamifu ya lugha katika Chuo Kikuu cha Ghana mwaka 2009 na sasa anafunza katika chuo cha elimu ya Kiafrika.

Tangu alipohamia Ghana, amegundua hajihisi kuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi wala kutukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake.

Anaelezea kuwa marafiki zake pia walijihisi hivyo walipohama Marekani.

Kambon sasa anaweza kuzungumza lugha mbili za Afrika Magharibi- Akan na Yoruba - anajaribu pia kuzungumza kidogo lugha ya Wolof.

Amekuwa akijifunza kusoma na kuandika Kiswahili ambayo ni lugha kuu katika eneo la Afrika Mashariki na pia inazungumzwa katika badhi ya sehemu za Kati na Kusini mwa Afrika.

Haki miliki ya picha Emmanuel Dzivenu/JoyNews
Image caption Obadele Kambon aliongoza kampeini ya kuondolewa kwa sanamu ya Mahatma Gandhi. katika Chuo Kikuu cha Ghana

Alifanya kampeini dhidi ya Gandhi

Amekuwa pia akijaribu kuanganzia masuala historia ya ukoloni kwa njia zingine.

Mwaka 2018, alifanikiwa kuongoza kampeini ya kuishinikiza Chuo Kikuu cha Ghana kuondoa sanamu ya kiongozi wa uhuruwa India Mahatma Gandhi.

Alisema ni bora kuweka sanamu ya kutambua mashujaa wa Kiafrika badala ya mtu ambaye aliwahi kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya raia wa Afrika Kusini- na alisema kuwa Wahindi walikuwa "bora kabisa" kwa watu weusi.

"Tukionesha kuwa hatujiheshimu au kudharau mashujaa wetu basi tutakuwa na tatizo ,"Bw. Kambon aliiambia BBC.

Japo utumwa ulifanyika kabla ya mwaka 1619, mwaka huo ulitajwa kuwa wa makumbusho ya miaka 400 tangu watumwa kwa kwanza wa kiafrika waliwasili nchini Marekani.

Makasri ya watumwa ya Elmina na Cape Coast katika pwani ya Ghana yalikuwa vituo vikubwa vya biashara ya watumwa ambapo amamilioni ya waafrika walitekwa na kuingizwa kwenye meli na kusafirishwa na hawakuwahi kurudi tena makwao.

Historia ya utumwa Marekani:

1619 - Watumwa wa kwanza wa Kiafrika waliuzwa Virginia na wakoloni wa Uingereza, japo watumwa walitumiwa na wakoloni wa Ulaya muda mrefu kabla ya hapo.

1788 - Katiba ya Marekani ilifanyiwa mabadiliko; na chini ya sheria hiyo mpya, watumwa walitambuliwa kama thuluthi tano ya mtu.

1808 - Rais Thomas Jefferson alikomesha rasmi biashara ya watumwa wa Kiafrika, lakini biashara ya watumwa wa ndani ilishamiri hasa katika majimbo ya kusini.

1822 - Wamarekani wenye asili ya Kiafrika waliochiliwa huru walikimbilia Liberia Magharibi mwa Afrika ambako waliopata makazi mapya.

1860 - Abraham Lincoln alikuwa rais wa Marekani; Jimbo la kusini lilijitenga hatua ambayo ilisababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka uliofuata

1862 - Rais wa Lincoln alitangaza kuwachilia huru watumwa wote katika majimbo yaliyotengwa.

1865 - Kusini iliposhindwa katika vita ; katiba ilifanyiwa marekebisho kwa mara ya 13 kufuta rasmi utumwa.

1868 - Marekebisho ya katiba ya 14 ilitoa nafasi kwa Wamarekani weusi kupewa uraia.

1870 - Marekebisho ya 15 ya katiba iliwapatia Wamarekani weusi wa kiume uhuru wa kupiga kura; huku majimbo ya kisini yakianza kupitisha sheria ya utengan.

Haki miliki ya picha Smith Collection/Gado

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ametangaza mwaka 2019 kuwa "Mwaka wa kurudi", akiongeza kuwa ni jukumu la nchi "kuwarudisha nyumbani" Waafrika ambao familia zao zililazimishwa kwa utumwa.

Mamlaka ya utalii imefanya matamasha kadhaa kuangazia uzuri wa taifa hilo kwa lengo la kuimarisha sekta yake ya utali.

Bw. Kambon anakaribisha mpango huo lakini ametoa wito kwa wa afrika wanaoishi ughaibuni kutotumiwa kama ''mtambo wa kuchuma fedha''.

Hata hivyo rais anachukulia suala hilo tofauti akiongeza kuwa ni fursa ya kuimarisha uhusiano wa nchi hiyo Marekani na kuwashawishi watu wanaotaka kuhama uwezekanao wa wao kuhamia Ghana - kitu ambacho viongozi wa kupigania haki Marcus Garvey na WEB Du Bois walikampeinia miaka ya 1920.

Du Bois alifanya Ghana kuwa nyumbani kwake na alifariki nchini humo mwaka 1963 akiwa na umri wa mika 95. Alizikwa mjini Accra.

Martin Luther King, Malcolm X na Muhammad Ali wote walifanya ziara ya ngazi ya juu nchini Ghana kwa lengo la kukumbuka mizizi yao Afrika.

Ghana inajivunia kuwa mwanzilishi wa umoja wa Afrika, mwanzilishi wake Kwame Nkrumah, alitangaza kuwa "Black Mecca", na kuonesha uungwaji mkono wake kwa Marcus Garvey kurejea Afrika katika miaka ya 1960.

Viongozi kadhaa wameendeleza na utamaduni huo - kwa mfano mwaka 2001 aliyekua rais wa Ghana wakati huo John Kufuor alipitisha sheria ya kuwapa makazi waafrika wanaoishi ng'ambo kuhamia Ghana.

Mwaka 2016, Bw Kambon - pamoja na Waafrika wengine thalathini na watatu wanaoshi nje ya nchi hiyo- walimuomba rais John Mahama, kuwapa uraia wa nchi hiyo.

Katika hatua yake ya mwisho madarakani kabla ya kushindwa katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwak huo, Bw. Mahama alitumia mamlaaka yake ya urais kuridhia ombi lao.

Haki miliki ya picha Obadele Kambon
Image caption Obadele Kambon ametumbuliwa na viongozi wa kitamaduni wa Ghana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii