Mkutano wa G7: Viongozi wa mataifa yenye nguvu wautafutia moto wa Amazon suluhu

An aerial view of forest fire of the Amazon taken with a drone is seen from an Indigenous territory in the state of Mato Grosso, Haki miliki ya picha Amnesty Handout via Reuters

Viongozi wa mataifa 7 tajiri zaidi duniani ambayo yamekutana katika mkutano wa G7 wameripotiwa kukaribia kukubaliana kusaidia kuzima moto katika msitu wa Amazon.

Rais wa Ufaransa,Emmanuel Macron amesema hayo siku ya jumapili wakati wakiwa wanajadili namna ya kutoa msaada wa kifedha na kiutaalamu.

Viongozi kutoka Marekani , Japan, Ujerumani, Italia, Uingereza na Canada wanaendelea na mkutano huo hii leo katika mji Biarritz uliopo maeneo ya ufukweni .

Mkutano umekuja wakati ambao mataifa yakiwa yana mvutano juu ya moto ambao umekuwa ukiwaka mara kwa mara nchini Brazil.

Rais wa Brazil,Jair Bolsonaro amekosolewa kwa kushindwa kutunza mazingira ya msitu wa Amazon na kutochukua hatua kwa watu wanaoharibu mazingira hayo.

Hali ya janga la moto huo na majibu ya serikali ya Brazil , umesababisa mataifa kupigia kelele na watu kuandamana .

Wiki iliyopita Rais Macron aliuelezea moto huo kuwa janga la kimataifa na kusisitiza mataifa hayo saba yenye nguvu duniani kutoa kipaumbele kutatua tatizo hilo.

Siku ya jumapili alisema kuwa viongozi wamekubaliana kusaidia nchi zote ambazo zimeathirika na moto huo haraka iwezekanavyo.

"Kikosi chetu kinafanya mawasiliano na nchi zote za Amazon na sasa tunamalizia hatua za mwisho muhimu zinazohusisha rasilimali za kiufundi na ufadhili ."

Waziri mkuu wa Uingereza,Boris Johnson alisema kuwa Uingereza iko tayari kuchangia paundi milioni 10 ili kulinda msitu wa Amazon ambao unasaidia uwepo wa mvua .

Ni hatua gani ambayo Brazil imeichukua?

Siku ya Ijumaa, kutokana na msukumo mkubwa kutoka katika nje ya nchi hiyo, rais Bolsonaro alitaka jeshi la nchi hiyo kusaidia kuzima moto huo.

Waziri wa ulinzi amesema kuwa kuna vikosi 44,000 ambao wako tayari kusaidia , na mamlaka imesema kuwa vikosi vya mataifa saba vimeidhinishwa kusaidia .

Ndege za kivita pia zimeagizwa kumwaga maji katika maeneo yote yaliyoathirika.

Rais wa Brazil aliandika katika ukurasa wake wa tweeter jana na kusema kuwa amekubali msaada uliotolewa na waziri mkuu wa wa Israel, Benjamin Netanyahu .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano nchini Brazil yanaendelea yakitaka usaidizi wa kimataifa

Rais Bolsonaro aliwahi kukosolewa na mataifa ya kigeni dhidi ya kauli yake ya kuyashutumu mataifa ya kigeni kuingilia uhuru wa taifa lake.

Rais huyo akitangazia umma kupitia kipindi cha telesheni namna ambavyo jeshi litasaidia kuzima moto , na kudai kuwa hawezi kutumikia kwa mujibu wa vikwazo vya kimataifa.

Siku ya jumamosi , muwakilishi kutoka Umoja wa ulaya Donald Tusk alikiri kuwa ni ngumu kuweka vizuizi vya kibiashara nchi za kusini mwa Marekani wakati Brazil ikiwa bado inashindwa kukabiliana na janga la moto inayoikabili nchi hiyo.

Wengine waliendelea kukosoa wiki iliyopita, waziri wa fedha nichini Finland alienda mbali zaidi na kuutaka Umoja wa Ulaya kufikiria kupiga marufuku uuzwaji wa nyama kutoka Brazil.

Chanzo cha moto ni nini?

Moto wa mwituni mara nyingi hutokea kipindi cha ukame na jua kali, lakini pia inawezekana na matokeo ya shughuli ya kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Ricardo Mello mkuu wa WWF Amazon amesema kuwa moto umesababishwa na ukwataji miti uliokithiri katika kipindi cha hivi karibuni.

Zaidi ya majanga 75,000 yamerikodiwa nchini Brazil kwa mwaka huu, na yote yakiwa yanatokea maeneo ya Amazon.

Wanaharakati wa masuala ya mazingira wanahusisha utendaji wa rais Bolsonaro dhidi ya majanga kadhaa ya moto yaliyotokea katika msitu huo ambao ni chanzo cha mvua.

Rais Bolsonaro ameshutumiwa kwa kutowachukulia hatua wachimba madini na wakata miti ambao huwa wanasababisha majanga haya ya moto jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Nchi ya jirani ya Bolivia pia imeathirika na moto huo.

Msitu wa Amazon una umuhimu gani?

Amazon ni msitu mkubwa duniani ambao ni chanzo cha mvua ambao unatunza kaboni ambayo hupunguza kasi ya ongezeko la joto duniani.

Msitu huo umezunguka nchi kadhaa lakini eneo kubwa liko Brazil.

Msitu huo unajulikana kama mapafu ya dunia kutokana na kazi yake ya kupunguza hewa ukaa na kutengeneza oksijeni.

Msitu huo ni makazi ya mimea na wanyama milioni tatu pamoja watu milioni moja.

Viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wadau wa mazingira ni miongoni mwa watu ambao wametaka hatua za kulinda msitu huo zichukuliwe hatua.

Maelfu ya waandamanaji pia wameonekana mtaani katika maeneo mbalimbali duniani wakitaka serikali ziingilie kati kutatua janga hilo.

Siku ya jumapili, Papa Francis pia aliunga mkono kampeni hiyo ya kulinda msitu huo.

"Tuna hofu pia dhidi ya janga la moto unaondelea katika msitu wa Amazon.

Tuombe Mungu asaidie kila mmoja atimize majukumu yake kwa ajili ya manufaa ya ulimwengu, tutafanikiwa punde" Papa aliwaambia maelfu ya watu katika makutano ya kanisa la mt. Petro.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii