Kaburi kubwa zaidi la watoto waliotolewa kafara lagunduliwa

Handout picture released by Programa Arquelogico Huanchacho on August 27, 2019 showing remains of some 227 children, allegedly offered in a sacrifice Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jamii ya Chimú ilikuwa ikitumia kafara kama sehemu ya ibada

Wanaakiolojia nchini Peru wamegundua kile kinachoaminika kuwa ni kaburi kubwa zaidi duniani la pamoja la watoto ambao walitolewa kafara na jamii yao.

Miili 227, ya kati ya miaka mitano mpaka 14 iligunduliwa karibu na mji wa pwani wa Huanchaco, kaskazini mwa mji mkuu wa Peru wa Lima.

Watoto hao inaaminika walitolewa kafara miaka 500 iliyopita.

Ugunduzi wa safari hii umekuja mwaka mmoja baada ya kugundulika makaburi yenye miili 200 ya watoto katika sehemu mbili tofauti nchini humo.

Wanaakiolojia wameliambia shirika la habari la kimataifa la AFP kuwa baadhi ya miili iliyofukuliwa hivi karibuni ilikuwa ingali na nywele na ngozi.

Watoto hao wanaonesha dalili ya kuwa waliuawa katika msimu wa mvua, na walizikwa mkabala na bahari ili kuwaridhisha miungu ya kiasili ya Chimú.

Haina uhakika wa moja kwa moja mauaji hayo yalitokea.

Jamii ya Chimú imeishi kaskazini ya pwani ya Peru na ilikuwa ni moja ya jamii zenye nguvu gani zaidi. Jamii hiyo ilikuwa na nguvu zaidi kati ya mwaka 1200 na 1400 kabla ya kupigwa na jamii ya Incas, ambao nao baadae walitawaliwa na Wahispania.

Haki miliki ya picha AFP

Walikuwa wakiabudu mungu mwezi waliemuita Shi ambaye waliamini ana nguvu kuliko jua. Waumini walikuwa wakitumia kafara ya watu hususani watoto kila walipokuwa wakifanya ibada.

Ufukuzi wa makaburi ungali unaendelea kwenye eneo hilo na wanaakiolojia wanaamini huenda miili zaidi ikagunduliwa.

"Ni kitu ambacho hakidhibitiki, hiki kitu cha makaburi ya watoto," mwanaakiolojia mkuu ameiambia AFP. "Kila unapochimba, kuna mwili mwengine".

Haki miliki ya picha AFP

Mada zinazohusiana