Utafiti: Mbinu mpya ya kukabiliana na msongo wa mawazo wakati wa ujauzito wagunduliwa

Stock image of woman holding a baby Haki miliki ya picha Getty Images

Karibu watu milioni 450 duniani wanakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo, hali inayofanya wengi wao kupata matatizo ya kiafya.

Baadhi ya watu hao wanakabiliwa na wakati mgumu kutafuta matibabu kutokana na unyanyapaa unaohusishwa na matatizo ya kiakili.

Wanawake wajawa wako katika hatari zaidi ya kufariki au kupoteza watoto wao wanapojipata katika hali hiyo.

Nchini Kenya kwa mfano, dalili za msongo wa mawazo kama vile uchovu na kupotelewa na usingizi wakati mwingine huchukuliwa kama dallili za ujauzito, na wakati mwingine husingiziwa kuwa uchawi.

Ukosefu wa huduma za Afya na viwango vya juu vya mzozo wa kinyumbani ulichangia 0.5% ya vifo vya kinamama wajawazito nchini humo mwaka 2015.

Msongo wa mawazo baada ya kujifungua pia unahusishwa na kuzaa mtoto mwenye uzani wa chini, mama kuwa mgonjwa au kupata matatizo wakati wa kunyonyesha.

Haki miliki ya picha African Academy of Sciences
Image caption Wanawake wengi katika maeneo ya vijijini nchini Kenya hutafuta huduma ya wakunga wa jadi

Kenya ina wataalamu wawili pekee wa afya ya akili kwa kila watu 100,000 na wote wanapatikana maeneo ya mijini.

Hii inamanisha kuwa baadhi ya maeneo ya vijijini ambako wanaishi mamilioni ya watu hawana mtaalamu wa magonjwa ya akili.

Inakadiriwa kuwa 75% ya watu walio na matizo ya kiakili wanaoishi katika maeneo vijijini hawana uwezo wa kupata matibu.

Hali inayowafanya kutafuta usaidizi wa waganga wa kienyeji na wafanyikazi wa afya badala ya wataalamu waliohitimu.

Watafiti waligundua kuwa ipo haja ya kuwapa mafunzo zaidi kundi hilo la watu katika jamii kutasidia kupunguza idadi ya watu walio na matatizo ya kiakili amabo haana uwezo wa kupata matibabu.

Ili kuimaririsha matokeo ya utafiti huo wakunga wa kienyeji walijumuishwa katika mafunzo hayo ili kuwabaini kinamama wajawazito walio na msongo wa mawazo.

Zaidi ya wanawake waja wazito 1,700 walihusishwa katika utafiti huo uliofanywa na Shirika la utafiti wa afya ya akili barani Afrika.

Utafiti huo amabo ulifanywa katika eneo la Kusini Mashariki mwa Kenya uliangazia zaidi maeneo yanayokaliwa na watu masikini yasiokuwa na mtaalamu yeyote wa masuala ya Kisaikolojia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafugaji katika eneo la Makueni Mashariki mwa Kenya

Mkunga wa jadi ni nani?

  • Mkunga wa jadi mara nyingi ndio sehemu ya kwanza ya mawasiliano kwa wanawake wajawazito katika maeneo ya vijijini Afrika
  • Japo hawajapewa mafunzo ya kimatibabu wanatekeleza jukumu sawia na wakunga wa kisasa
  • Wanajifunza kazi kupitia uwanagenzi na wakati mwingine wanapokea ada kutoka kwa familia ya mama mjamzito
  • Kando na kuwasaidi kinamama kujifungua pia wanawapa ushauri wakati wanapojiandaa kuwa mama kwa lengo la kupunguza mzozo wa kinyumbani.
  • Wakunga wa wa kienyeji walitumia muongozo wa Edinburgh kukabiliana na msongo wa mawazo baada ya kujifungua kuwauliza maswali kinamama waliojifungua hospitali na nyumbani.

Mzozo wa nyumbani

Matokeo ya uchunguzi huo yalikuwa ya kushangaza

Robo ya kinamama walishirikishwa katika utafiti huo walipatikana na matatizo kidogo ya usumbufu wa akili.

Thuluthi tatu walinyanyaswa na wapenzi au waume zao iwe ni kingono au kisaikolojia.

Karibu 60% ya kinamama hao walipatikana na msongo wa mawazo na kupewa matibabu na wakunga wa jadi kulingana na mwongozo wa tiba wa Shirika la Afya Duniani uliotolewa kwa watu wasiokua wataalamu wa matibabu.

Haki miliki ya picha African Academy of Sciences
Image caption Baadhi ya majukumu ya wakunga wa jadi ni kuwashauri kinamama wajawazito kuhusu changamoto za uzazi na familia

Kinamama hao walikuwa na umri wa miaka 26 huku wengine walioshirikishwa katika utafiti huo wakiwa na umri wa kati ya miaka 12 na 24.

Mooja wao alikuwa, Ndanu,amabye alipatikana na tatizo la kiakili.

Anasema : "Laiti mpango huo haukuwepo na na si kupata huduma ya mkunga wangu, Ningelimpoteza mwanangu kwa sababu sidhani ningelienda kliniki.

"Mkunga alinishauri nitunze afya yangu na ya mtoto wangu kwa kuhakikisha nafika kliniki kama ilivyopangwa. Aliniahidi kuwa mlango wake upo wazi wakzti wowote natajihisi kusema nae"

Haki miliki ya picha African Academy of Sciences
Image caption Mafunzo ya afya ya akili yalizingaztia mwongozo wa WHO kwa watu wasiokuwa wataalamu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii