Kwa nini India imewavua uraia watu milioni 1.9?

Watu milioni 4 walivuliwa uraia katika rasimu ya kwanza ya sajili ya kitaifa iliotolewa mwezi Julai mwaka huu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu milioni 4 walivuliwa uraia katika rasimu ya kwanza ya sajili ya kitaifa iliotolewa mwezi Julai mwaka huu

India imechapisha orodha ya mwisho ya watu milioni 1.9 iliyowavua uraia wake Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Sajili ya kitaifa ya raia(NRC)ni orodha ya watu ambao wanaweza kuthibitisha kuwa waliinga nchini humo kufikia mwezi 24 Machi mwaka 1971, kabla ya Bangladesh kupata uhuru wake kutoka kwa Pakistan.

Watu ambao hawajajumuishwa katika sajili hiyo wana siku 120 kukata rufaa dhidi ya hatua ya kuvuliwa uraia wa nchi hiyo.

Haijabainika nini kitakachofuata baada ya hatua hiyo kutekelezwa.

India inasema mpango huo ni muhimu katika mchakato wa kuwabaini wahamiaji haramu kutoka Bangladesh.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption NRC ilibuniwa mwaka 1951 kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.

Tayari maelfu ya watuwaliokamatwa wanazuiliwa katika kambi ya muda kwa kushukiwa kuwa raia wa kigeni, lakini kuna hofu ikiwa watakubalika walikotoka.

Mpango huo umezua gumzo kali baadhi ya watu wakidai ni"hujuma" dhidi ya jamii ya Assam walio wachache.

Rasimu ya sajili hiyo iliyochapishwa mwaka jana iliwatenga watu milioni nne.

Sajili ya Kitaifa ya raia ni nini?

Sajili ya NRC ilibuniwa mwaka 1951 to kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.

Sajili hiyo imefanyiwa mabadiliko kwa mara ya kwanza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Saheb Ali, 55, mkazi wa Wilaya ya Goalpara amevuliwa uraia

Familia katika jimbo la Assam wamekuwa wakitakiwa kuwasilisha stakabadhi zinazo thibitisha kuwa ni wazawa wa nchi hiyo huku wale wanaoshindwa kufanya hivyo wakichukuliwa kuwa wahamiaji haramu

Chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kwa muda mrefu kimekuwa kikipinga uhamiaji haramu nchini humo lakini miaka ya hivi karibuni kimeipatia kipaaumbelea sajili ya kitaifa ya raia NRC.

Kwa kuhofia huenda wakavuliwa uraia na badae kufungwa jela maelfu ya Wahindu wa Bengali na Waislamu wamejiua tangu mpango wa kusafisha Sajili ya uraia ulipoanza mwaka 2015 baadhi ya watu wamejitoa uhai, anasema mwanaharakati.

Baadhi ya watu waliozuiliwa wanalalamikia hali mbaya ya maisha katika vituo vya kuwashikilia wale wanaodaiwa kuwa wahamiaji haramu ambavyo vimejaa kupita kiasi.

Mahakama maalumu za kusikiliza kesi za uraia nchini India zilibuniwa mara ya kwanza mwaka 1964 na tangu wakati huo mahakama hiyo imeamua kuwa zaidi 100,000 ni raia wa kigeni.

Lakini uamuzi wa mahakama hizo zimekumbwa na utata kutokana na jinsi zinavyoendeshwa.

Suala la kubaini ikiwa mtu ni mzawa wa India au mhamiaji haramu limekuwa likizua utata kwa kuwa familia nyingi hazina stakabadhi hali inayotokana na ukosefu elimu wengi wao hawatilii maanani umuhimu wa kutunza nyaraka.

Wengine hawana fedha za kuwasilisha madai hayo kesi mahakamani ili wapate ufumbuzi wa kisheria

Kwa nini sajili hiyo inatumika Assam?

Assam ni moja ya majimbo ya India inayokaliwa na watu kutoka jamii tofauti na suala la uraia wao limekuwa likitiliwa shaka kwamuda mrefu.

Miongoni mwa watu hao ni jamii ya Bengali na Assamese-wanaozungumza kihindi.

Thuluthi tatu ya watu milioni 32 million wanaoishi katika jimbo hilo ni Waislamu, idadi ambayo ni yapili kwa ukubwa baada ya wale wanaoishi Kashmir.

Wengi wao wametokana na kizazi cha wahamiaji walikalia eneo hilo wakati wa utawala wa Uingereza.

Lakini wahamiaji haramu kutoka taifa jirani la Bangladesh, ni kilomita 4,000- kutoka mpaka wa India, wamekuwa wakuwa wakiishi kwa hofu kwa miongo kadhaa sasa.

Mwaka 2016 serikali ilitangaza kuwa inakadiria karibu watu milioni 20 wanaoishi India ni wahamiaji haramu..

Je kuna kundi linalolengwa kwa misingi ya kidini?

Watu wengi wanasema mpango huo hauna uhusiano wowote na masuala ya kidini, lakini wanaharakati wa kutetea haki wanadai kuwa jamii ya Bengali ambao wengi wao ni waumini wa dini ya Kiislamu, ndio wanaolengwa.

Pia wanahofia hali ya Waislamu wa jamii ya Rohingya walio wachache katika taifa jirani la Bangladesh.

Hata hivyo wahindi kadhaa wanaozungumza Kibengali-wameachwa nje ya sajili ya kitaifa ya uraia hali ambayo imezua taharuki katika Jimbo la Assam

"Moja ya jamii iliyathiriwa zaidi na mpango huu ni Wahidu wa Bengali. Wengi wao wamekamatwa na kuzuiliwa kambini. Hii ndio sababu siku chache kabla ya NRC kuchapishwa BJP ilibadili mkondo wa mchakato huo ikisema kuwa inakiri kosa lilifanyika katika uchapishaji wa orodha hiyo ya mwisho. Hii ni kwasababu Wahidu wa Bengali ni wafuasi sugu wa BJP," anasema Barooah Pisharoty.

Watu ambao majina yao hayapo katika sajo ya kitaifa wanaweza kukata rufaa katika mahakama maalum iliyobuniwa kusikiliza kesi yao.

Pia wanaweza kuwasilisha kesi katika mahakama kuu au Mahakama ya Juu zaidi.

Haki miliki ya picha Citizens for Justice and Peace
Image caption Baba na mwanawe waliwahi kujitoa uhai kutokana na suala la uraia wao

Kuna hofu rufaa hizo zitachukua muda mrefu kuamuliwa hali ambayo itasababisha msongamano zaidi mahakamani huku familia masikini zikikabiliwan a wakati mgumu kutafuta fedha za kupigana kisheri kuhusu kesi ya uraia wao.

Watu watakaopoteza rufaa waliowasilisha huenda wakafungwa jela.

Watu 1,000 waliothibitishwa kuwa raia wa kigeni wamekuwa wakizuiliwa kwa miezi sita sasa katika jela za India.

Serikali ya Nerendra Modi pia inajenga jela mpya itakayoweza kuwa na uwezo wa kuwazuilia hadi watu 3000.

"Watu ambao majina yao hayapo katika sajili ya uraia wamekuwa wakiishi kwa hofu wasijue hatma yao ni ipi," Sangeeta Barooah Pisharoty, mwandishi wa Assam wa kitabu: The Accord, The Discord, aliiambia BBC

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hatua ya kuvuliwa uraia kwa watu hao inatarajiwa kusababisha maandamano kmakubwa

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii