Vatcan: Papa Francis achelewa kanisani baada ya kukwama kwenye lifti

Papa Francis Haki miliki ya picha Reuters

Papa Francis ameomba radhi kwa kuchelewa misa katika kanisa la Mt. Petro na kusema kuwa alikwama kwenye lifti akiwa anaelekea kanisani.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 alikwama kwenye lifti kwa dakia 25 mara baada ya umeme kukatika na kuweza kutoka kabla ya kikosi cha wazima moto hakijawasili.

"Ninapaswa kuomba radhi kwa kuchelewa," Papa huyo aliawaeleza waumini wake huku akitabasamu.

Na kuwataka waumini wote kuwapongeza wazima moto kwa kazi kubwa waliofanya .

Papa akiwahutubia umati wa watu kusema "kumekuwa na itilafu ya umeme hivyo lifti ilisimama".

"Namshukuru Mungu na kikosi cha zima moto kilifika kwa wakati "

Televisheni inayorusha matangazo ya moja kwa moja ya sala hiyo walihisi papa huyo amechelewa kufika katika misa kutokana na sababu za kiafya, shirika la habari la AFP limeripoti.

Papa huyo alitangaza pia kuwa mwezi ujao, atatangaza makadinari 10 wapya wa kanisa katoliki.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii