Miraji Mtaturu aapishwa rasmi kuwa mbunge wa Singida Mashariki
Huwezi kusikiliza tena

Miraji Mtaturu aapishwa rasmi kuwa mbunge wa Singida Mashariki

Miraji Mtaturu, kutoka Chama Cha Mapinduzi, CCM, ameapishwa rasmi hii leo kuwa mbunge wa Singida Mashariki.

Mtaturu anachukua kiti hicho cha ubunge ambaho awali kilishikiliwa na Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge wake na Spika Job Ndugai mnamo Juni 28 mwaka huu.

Mtaturu alitangazwa mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kupita bila ya kupingwa katika hatua za awali za matayarisho ya uchaguzi mdogo baada ya wagombea 12 wa vyama vya upinzani kutorejesha fomu.

Uchaguzi huo mdogo ulikuwa ufanyike Julai 31, lakini haukufanyika tena kutokana na wapinzani kutokurejesha fomu zao.

Hata hivyo, kuna kesi mahakamani ambayo inaweza kuathiri kiapo cha Mtaturu hii leo pale ambapo maamuzi yake yatakapotolewa wiki ijayo.

Kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lissu akipinga kuvuliwa ubunge wake.

Mada zinazohusiana