Justin Bieber aweka wazi jinsi umaarufu ulivyoathiri maisha yake

Justin Bieber Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bieber ameweka wazi jinsi alivyokuwa anasumbuliwa na sonona

Mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko ya Pop ameandika ujumbe mrefu wa hisia kuelezea namna alivyoingia kwenye uraibu wa dawa za kulevya na kusababisha dunia imchukie.

Bieber anadai alijikuta katika vitendo hivyo kutokana na maamuzi mabaya aliyofanya wakati akiwa na miaka 20.

Nyota huyo ambaye aliibuliwa na meneja wa muziki Scooter Braun akiwa na umri wa miaka 13 amekiri kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa sana na kupelekea kutokuwa na mahusiano mazuri na watu .

"Nilianza kuwa mtu mwenye hasira na kuwanyanyasa wanawake," aliandika.

"Nilianza kujiweka mbali na kila mtu ambaye alinipenda...nilihisi kama vile siwezi kurudi katika hali yangu ya zamani"

Nyota huyo wa Canada alikuwa anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili ameeleza namna alivyokuwa .

"Nilianza kupata umaarufu duniani kote nikiwa na miaka 13 akiwa anatokea katika mji mdogo,

akiwa na mamilioni wa mashabiki wakieleza namna ambavyo wanampenda na wanapenda muziki wake," alisema.

"Ukisia mambo kama hayo ukiwa kijana mdogo lazima uanze kuamini."

"Kila mtu alifanya kila kitu kwa ajili yangu, hivyo sikuweza kujifunza kuwajibika kwa ajili ya maisha yangu".

Jinsi matatizo yalivyoanza

"Nikiwa na miaka 18, nilikuwa na mamilioni ya fedha katika akaunti na nilikuwa na uwezo wa kupata kila kitu nilichokuwa nnakitaka, sikujua katika ulimwengu".

Bieber anasema kuwa akiwa na miaka 19, alikuwa anatumia dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa na kuwa na mahusiano yenye mgogoro.

"Nilifanya kila maamuzi mabaya ambayo unaweza kuyafikiria na kubadilika kutoka mtu aliyependwa zaidi na kuwa mtu anayehukumiwa na kuchukiwa na kila mtu duniani".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bieber amemsifia mke wake Hailey Baldwin, kwa kumsaidia kurudisha uhai wa maisha yake

Bieber aliwahi kushikiliwa na polisi mara kadhaa mwaka 2014 kwa kosa la kutokuwa makini katika uendeshaji gari .

"Iliniwia vigumu kuamka asubuhi… nilihisi kama nnaenda kukutana na matatizo kila kona," aliandika.

"Kuna wakati ulifikia ambao nilikuwa sitamani kuishi tena.

Kwa sababu nilihisi hiyo hali haiwezi kuisha."

Hata hivyo nyota huyo amesema kuwa imani yake ya kikristo na msaada aliopata kutoka kwa marafiki na familia pamoja na mke wake wameweza kumsaidia kurejesha maisha yake.

"Ilinichukua miaka kupambana na maamuzi hayo mabaya , kubadili mwenendo wangu katika mahusiano" aliandika Bieber.

"Lakini kwa bahati nzuri Mungu alinipa watu ambao walinipenda mimi kama mimi na sasa ninafurahia maisha yangu ya ndoa!!"

Ujumbe huo wa Instagram ulimiminika kwa maoni ya mashabiki wake wakimuuunga mkono na kuonyesha upendo kwake.

"Makosa yalifanyika lakini nimeweza kuipata njia ya kurudi katika sehemu nzuri, ninajivunia kuwa Belieber."

Nimepitia changamoto ya kuwa nyota katika umri mdogo lakini nimeweza yashinda yote na kwa moyo wote na akili kusonga mbele.

Mnamo mwaka 2014, wanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 20, alituhumiwa kwa kosa la kumuibia mwanamke mmoja ambaye ni shabiki wake.

Kulingana na mtandao wa taarifa za wasanii wa kimataifa, TMZ, Bieber anatuhumiwa kumnyang'anya mwanamke huyo simu yake.

Inaarifiwa mwanamke huyo alikua ametumia simu yake kumpiga picha Bieber .

Mwaka 2017, Justin Bieber alihusika katika ajali iliofanyika eneo la Beverly Hills na kukaatwa na maafisa wa polisi.

Kanda ya video imeonyesha mwanamuziki huyo akimgonga mtu aliekuwa akitembea kwa miguu baada ya kutoka katika ibada ndani ya kanisa moja mjini Los Angeles.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii