Utamaduni wa kubana misuli ya uke ni hatari kwa wanawake

Shabu

Utamaduni wa wanawake kubana misuli ya uke umekuwa ukifanywa na jamii nyingi barani Afrika katika miaka mingina katika pwani ya Afrika mashariki hasa jamii ya waswahili wamekuwa wakipokezana utamaduni huu kutoka kizazi kimoja hadi kingine lakini katika miaka ya hivi karibuni hasa katika miji mikuu kama vile Mombasa, wanawake wamekuwa wakitumia mbinu nyingine ambazo ni za kisasa japo huenda zikahatarisha maisha yao.

Ukipita mtaa wa Likoni Jijini Mombasa, pwani ya Kenya, utamaduni huu wa wanawake kubana njia zao za uzazi si geni.

Munira Ali Salim ni mkaazi wa Mombasa na kama wanawake wenzake anaelewa Faida zake. Na wanachotumia zaidi kwa shughuli hiyo wenyewe wanaita shabu.

Je wanawake wote wanafika kileleni?

Hatari ya 'tiba ya ukarabati' wa uke

''Hii shabu husaidia maana yake kuna wengine humwaga maji sana. Sasa hii shabu shabu ukitia huko, humfanya mtu mkavu halafu huvuta na ikabana''. Munira

Hasa ndicho kinacho wahangaisha wanawake hawa wa Mombasa. Baadhi yao wana wasi wasi kuwa uke wao ni mpana kiasi kuwa hawa toshlezi waume wao.

Na ndio maana wanatumia hii shabu kujaribu kubana ili kurudisha ile hali ya zamani.

Lakini hapa mbinu wanazo tumia zinahusisha bidhaa za kemikali wanazonunua dukani.

''Hii ndio shabu na kazi yake ni kuchukua hiki kipande unaponda kisha unafunga kwenye pamba. Na unachanganya na mafuta mazito yenye harufu nzuri mfano manukato ya Udi. Sasa hiyo inasaidia ukitia huku chini shabu inavuta''

Wanawake hawa pia wameelezea hofu kuwa waume huenda wakawaacha au kuwatafutia mke wa pili iwapo wata kosa kuridhika nao kimapenzi. Na yote haya wamejifunza kutoka kwa makungwi ambao huwapa ushauri nasaha wasichana wanapo olewa, kuhusu njia za kumridhisha na mume .

Mbali na shabu ambayo inatengenezwa kwa chumvi, kuna bidhaa nyingi zinazopatikana madukani kama vile choki, inayotengenezwa kutoka kwa chokaa maalum yenye kemikali inayoaminiwa kuvuta misuli ya uke na kubana.

Madhara ya matumizi ya bidhaa hizi kwa wanawake

Bidhaa hizi wanazonunua hawajui zimetokana na kitu gani na wala hazina maelezo ya namna ya kutumia na wala hakuna ushauri wa daktari wala hawana hofu kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza hapo baadae.

Daktari Kinuthia Muriu ni mtaalamu wa afya ya uzazi anasema matumizi ya bidhaa hizi yapo sana miongoni mwa jamii ya wanawake.

''Kwa makabila fulani huwa wana njia nyingi wanatumia kubana njia ya uzazi, nyingine ni mbaya huweka mpaka chumvi inayounguza mwili hali ambayo baadae huwa kuna madhara. kuna wale wanapata msukumo kutoka kwa jamii, fikra zao wanaona kama wana maumbo yaliyo na shida, wanahitaji ushauri nasaha ili waweze kujikubali''.

Daktari Muriu anasema kuna njia mbalimbali zinazotumika kisayansi zinakubaliwa ili kuandaa mwili wa mzazi kwa mfano wakati wa kuuandaa mwili na kurekebisha mwili kama kubana njia za uzazi na wengi hufuatilia matibabu hayo, kuna mazoezi kama yale kitaalamu yanaitwa Kegel, mazoezi yanayosaidia kurejesha maumbile ya mwanamke.

Mada zinazohusiana