Siku ya kuzuia vitendo vya kujiua 2019: Unawezaje kuzungumza na mtu mwenye mawazo ya kujiua?

Mawazo ya kujiua huwakumba watu wa rika zote Haki miliki ya picha Getty Images

Kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja mahali fulani, wanajikatiza uhai duniani.

Watu takribani 800,000 hufa kwa kujikatiza uhai wao kila mwaka kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO) na ni sababu ya pili ya vifo miongoni mwa watu wenye umri kati ya miaka 15 na 29, nyuma ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.

WHO inasema kuwa tatizo hili halijazungumzwa vya kutosha miongoni mwa jamii za watu.

Vitendo hivi huathiri watoto, wazazi, wenza na marafiki.

Katika siku ya kupinga vitendo vya kujitoa uhai, tunaangazia namna ambavyo tunaweza kuzungumza na mtu anayefikiria kujiua.

Anza mazungumzo

Haki miliki ya picha Getty Images

Hakuna namna nzuri au mbaya ya kuzungumza kuhusu hisia za kujiua- kuanza mazungumzo ni muhimu, Emma Carrington, msemaji wa taasisi ya Rethink ya Uingereza, ameiambia BBC.

''Kwanza tunapaswa kutambua kuwa ni mazungumzo magumu. Haya si mazungumzo kama tunayokuwanayo kila siku. Hivyo utaogopa na ni sawa kuwa na hofu, Muhimu ni kusikiliza bila kuhukumu''.

Jina ulilopewa lina maana gani?

Masaibu ya kuishi na jinsia mbili

Ni nani aliye hatarini?

Vitendo vya kujiua vinaathiri watu wa rika zote lakini vitendo vya kujitoa uhai kwa wanaume vimekuwa juu.

Mwaka 2016, idadi ya wanaume waliojiua walikuwa 13.5 miongoni mwa 100,000 na 7.7 kwa 100,000 miongoni mwa wanawake.

Hatahivyo uwiano wa wanaume na wanawake unatofautiana nchi na nchi.

Urusi iliongoza mwaka 2016 kwa kuwa na idadi kubwa duniani ya wanaume wanaojitoa uhai.

Lakini matukio haya hutokea zaidi yakati kunapokuwa na mizozo, au nyakati ambazo watu wanakuwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kifedha, kuvunjika kwa mahusiano, maradhi sugu na maumivu yasiyokwisha.

Idadi kubwa ya watu walio mjini hujiua, na makundi ya watu wanaokabiliwa na unyanyapaa,kama vile wakimbizi na wahamiaji, watu wa mapenzi ya jinsia moja na wafungwa.

Kwa mujibu wa WHO, sababu nyingine ni mizozo, majanga, machafuko, unyanyasaji, kupoteza wapendwa na kutengwa.

Haki miliki ya picha Getty Images

''Mtu anaweza kujihisi kutengwa hata kama anaonekana kuzungukwa na watu, isipokuwa tu kama watu hao ni msaada kwa mtu huyo vinginevyo mzigo unakuwa mkubwa'' ameeleza Carrington.

Jamii inaweza kufanya nini?

Shirika la WHO linasema serikali zinaweza kufanya jitihada nyingi kuondokana na vitendo vya kujiua:

  • Kuvunja unyanyapaa na kuzungumza kuhusu suala hilo.
  • Kuwasaidia vijana wadogo kuwa na ujuzi ili kukabiliana na changamoto za maisha.
  • Kuwasaidia wahudumu wa afya kwa kuwapa mafunzo ya kutathimini na kuzuia tabia zinazomfanya mtu kuwa kwenye hatari ya kujitoa uhai wake.
  • Kuwatambua watu walio kwenye hatari ya kujiua na kuwa na mawasiliano nao kwa muda mrefu.
Haki miliki ya picha Getty Images

Usihukumu

Si lazima uwe mtaalamu wa afya kumsaidia aliye hatarini.Unatakiwa kuwa mtu ambaye amejitayarisha kwa ajili ya kuzungumza, wanaeleza wataalamu.

Wakati kutafuta msaada wa wataalamu ni namna salama, Carrington anasema kuzungumza ukweli kuhusu kujiua kunaweza kuonesha kuwa hauhukumu.

Hicho kinaweza kufanya mtu kujihisi yuko salama kwa muda mfupi.