Raia wa Zimbabwe kuuaga rasmi leo mwili wake

Mwili wa Mugabe ukiwasili Haki miliki ya picha Reuters

Baada ya kuwasili kwa mwili wa Mugabe nchini Zimbabwe kuwasili kutoka Singapore, leo unatarajiwa kuagwa rasmi kabla ya kuzikwa Jumapili.

Mugabe, alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi mwaka 2017.

Atazikwa siku ya Jumapili baada ya shughuli za maziko siku ya Jumamosi.

Mwili wa Mugabe umepelekwa kwenye makazi ya familia ''Blue Roof'' mjini Harare.

Mipango ya maziko ikoje?

Siku ya Alhamisi na Ijumaa, Mwili wa Mugabe utalala katika uwanja wa mpira wa Rufaro eneo la Mbare mjini Harare, ambapo ndipo alipoapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Zimbabwe baada ya kupatiwa uhuru kutoka kwa koloni la kiingereza mwaka 1980.

Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi ,kwenye uwanja wenye uwezo wa kupokea watu 60,000 kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.

Rais wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa ametaja kuwa ''shujaa wa taifa'' kwa jitihada zake za kuisaidia Zimbabwe kupata uhuru wake.

Lakini ripoti zinasema kuwa Mugabe hakutaka waliomuondoa madarakani kushiriki katika maziko yake, hivyo badala yake huenda shughuli za maziko zikafanywa kwenye makazi ya familia yake.

Haki miliki ya picha Getty Images

Familia ya Mugabe inapinga mpango wa serikali wa kumzika katika makaburi ya mashujaa wa taifa katika mji mkuu wa Zimbabwe -Harare na wanataka azikwekwe katika kijiji alikozaliwa.

Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.

Mugabe ambaye anakumbukwa na wengi kama mkombozi ambaye aliwaondoa watu wake katika pingu za ukoloni wa wazungu walio wachache anakumbukwa na wengine kama mtu aliyeangusha uchumi wa moja ya chumi zilizotazamiwa kufanya vizuri zaid barani Afrika na ambaye aliwatesa kikatili wapinzani wake.

Robert Mugabe amefariki dunia

Kwa Picha: Enzi ya Mugabe mamlakani

Umaarufu wake

Alikuwa maarufu miongoni mwa wapiga kura wengi hata katika kipindi chake cha hivi karibuni alipoondolewa mamlakani.

Aliondolewa mamlakani alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye baadaye alikuwa rais wa taifa hilo.

Rais Emmerson Mnangagwana akimsifu Mugabe tangu habari za kifo chake zianze kutolewa.

Bwana Mnangagwa alisema kwamba chama tawala Zanu -PF kilimpatia hadhi ya ushujaa wa taifa aliyohitaji.

Mada zinazohusiana