Unyanyasaji wa kingono Afrika kusini: 'Nilibakwa sasa nawahofia mabinti zangu'

Sarah Midgley Haki miliki ya picha Sarah Midgley

Waafrika kusini wameghadhabishwa na msururu wa visa vya ubakaji na mauaji ya wanawake katika wiki za hivi karibuni - kikiwemo cha msichana wa shule aliyevunjwa fuvu la kichwa na mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepigwa kwa kifaa butu hadi kufariki.

Ubakaji na mauaji yamechangia maandamano na kampeni ya #AmINext campaign katika mtandao wa kijamii Twitter, na waraka uliotiwa saini na zaidi ya watu 500,000 kutaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo katika taifa linalokabiliana na viwango vya juu vya uhalifu.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ameahidi msururu wa hatua kukabiliana na mzozo - ikiwemo kuidhinisha daftari la wahalifu, kuongeza idadi ya "mahakama maalum ya wahalifu wa unyanyasaji wa kingono", na hukumu kali zaidi.

Mpiga picha Sarah Midgley, mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 37 anayeishi katika mji wa Johannesburg, bado anapata unafuu kutokana na athari za kubakwa tariban muongo mmoja uliopita.

Amemuarifu mwandishi wa BBC wa masuala ya wanawake Esther Akello Ogola kuhusu masaibu yake.

Nilibakwa na aliyekuwa mpenzi wangu mnamo 2010, karibu na muda wa wakati Kombe la Dunia lilipokuwa linafanyika Afrika kusini.

Mpenzi wangu alikuwa akininyanyasa kimwili na kiakili kwa takriban mwaka mmoja na nusu kabla nilipojiamini kuondoka.

Nilitishia kuondoka mara kadhaa lakini kila nilipojaribu , alinigeukia na kunishambulia zaidi.

Alinipiga mateke, mara nyingine ananikaba koo na kuniuma. Alitisha kuwabaka binti zangu mara kwa mara na kuwaua mbele yangu iwapo nitasubutu kumwacha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawake wengi na wasichana wanaishi wakiwa na hofu ya kubakwa

Sikumueleza mtu yoyote kuhusu hili kwasababu niliona aibu na kushikwa na haya kwamba sikuweza kujitetea.

Nilijitenga na familia na marafaiki kwasababu sikujiamini baada ya kupata talaka na mpenzi wangu huyo wa zamani alinishawishi kuwa rafiki zangu na familia yangu haikunijali. Niliamini pia kwamba atawadhuru watoto wangu.

Nilipoamini kumuacha hatimaye, niliondoka kwa siri. hatahivyo siku 10 baadaye alikuja kwangu.

Nilishtushwa pakubwa kwamba alinipata.

Alisema amekuja tu kuniomba msaada kwa mara ya mwisho. Alisema hana pesa wala uwezo wa kwenda shamabani kwa mjombake ambako ni kiasi ya 25km kutoka nilikokuwa naishi.

Aliniahidi kuwa ataniondokea maishani mwangu kabisa, iwapo nitampeleka kwa gari. Nilimuamini.

Kwa miaka mingi baad aya ubakaji huo, najilaumu kwa kuamini kwamba angeniacha huru.

Muda mfupi wakati tukiwa kwenye safari garini, nilihisi akibadilika. Alikuwana wasiwasi na nilijiambia pengine ni kutokana na kwamba yeye ni mraibu wa madawa ya kulevya aina ya heroin.

Nilimuambia nitafika mpaka kwenye langi tu la kuingia shamabni pekee alafu nitarudi zangu.

Kama nilidhani kwamba mambo sio salama, aliyofanya baada ya hapo yalithibitisha fikra zangu. Aliniambia ningeondoka iwapo tu ataniambia niodnoke na akafunga milango ya gari.

Nilipofika shambani, alikuja upande niliokaa na kufungua mlango na kunivuruta kwa nywele na nilipokuwa naanguka kutoka kwenye gari alinipiga teke kichwani na nikapoteza fahamu.

Nilipopata fahamu, nilikuwa kwenye moojawapo ya nyumba katika shamba hilo na alikuwa yuko juu yangu. rafiki yake mmoja pia alikuwa amekuja na kunibaka pia wakati mpanezi wangu huyo wa zamani alipomaliza.

Nilipotewa na fahamu tena na nilipoamka, mhudumu wa mjombake shambani humo alikuwa amekaa karibu na mimi na wao walikuwa wameondoka.

Huwezi kusikiliza tena
Je, kuna umuhimu wa kuzungumzia swala la ubaki waziwazi?

Ilibidi nitolewe kizazi

Mwanamke huyo mhudumu alikuwana ndoo ya maji na alikuwa anajaribu kunipangusa huku akijaribu kunifunika kwa nguo zake. Nilimuomba aache na apige simu polisi na aite ambulensi. Iliwasili ambulensi na na nikapelekwa hospitali.

Kwa bahati mbaya majeraha niliopata yalikuwani mabaya na ilibidi nitolewe kizazi.

wakati haya yakifanyika, niligundua kuwa aliyenibaka ameachiliwa kwa dhamana na alitoroka mjini. kwa miezi tisa niliishi kwa uoga.

Alikamatwa tena na kuhukumiwa miaka minane gerezani. Alifariki kutokana na saratani ya tezi ya kibofu cha mkojo mnamo 2017 akiwa ametimiza miaka saba ya kifungo chake.

kwa kweli naweza kusema hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza nilipopumua katika miaka 7. Sikuwasilisha kesi dhidi ya rafiki yake kwasababu sikuweza kupitia msongo nilioupata wakati wa kusikizwa kesi.

Nilikuwa noata ndoto mbaya kwamba mpenzi wangu huyo wa zamani atarudi na anishambulie mimi na watoto wangu.

Nilihama kwenda kuishi katika nyumba ya wazazi wangu, kwasababu sikuweza kuishi peke yangu.

Kwa bahati mbaya nawaogopa wanaume, najaribu nisilionyeshe lakini sidhani kama wanaume wanatambua namna wanavyoweza kumtishia mtu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raia Afrika kusini wanataka serikali idhibiti uhalifu huo

Niliingiwa na uoga kuhusu usalama wa mabinti zangu

Nimekuwa napokea matibabu kwa miaka, kwa kiasi fulani inayohusu athari za msongo wa utotoni, (Nilibakwa nikiwa mtoto)baada ya shambulio langu.

Kitu kibaya zaidi, kama muathiriwa wa ubakaji ambaye nimama wa mabinti, ni kushuhudia watoto wako wakipitia ulioyapitia.

Nitasononeka iwapo yalionifika mimi yakawafika wao.

Hivyobasi nimewafunza kwamba daima watajihisi salama watakapokuwa na mimi. daima wanaweza kuniamini, wana sauati wanayoweza kuitumia, na nitawaamini siku zote.

Niliingiwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wao. Niliwanunulia simu na nikawa najikuta nachunguza kila wanakokwenda, na kila ninapoeweza nilikwenda nao kokote walikotaka kwenda, hata kama ni kukaa na marafiki zao.

hatimaye niliishia kukabiliwa na mchoko na ikanibidi nirudi kupokea matibabu kujaribu kuacha kuwa na wasiwasi mwingi.

Binafsi sihisi kwamba hatua za kutosha zinachukuliwa Afrika kusini.

Watu hawaoni ukubwa wa hali imnayowakabili wanawake na kwa bahati mbaya baadhi ya wanaotoa sababu kwa mashambulio hayo ni wanawake wanaosema: "Kilichofanyika kimefanyika. Inabidi tusonge mbele na tuwe na matumaini."

Hilo sio suluhu kwa wanawake kubakwa na kuuawa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii