Watu 50 wanahofiwa kufariki Tanganyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya ajali ya treni

picture taken on April 22, 2014 shows derailed wagons after a train sped off the rails 65km north of Kamina, in the southern province of Katanga, Democratic Republic of Congo. Haki miliki ya picha NUMBI MATHYS
Image caption Picha hii ni ya Aprili 22 mnamo 2014 - katika ajali nyingine ya treni iliopoteza muelekea 65km kutoka Kamina jimboni Katanga katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika jimbo la Tanganyika huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya treni kupoteza muelekeo.

Waziri wa masuala ya kibinaadamu, Steve Mbikayi ameithibitishia BBC kuwa watu 50 wanahofiwa kufariki katika ajali hiyo.

Mbikayi ameelezea ajali hiyo kuwa janga jingine na kufahamisha kuwa mutano unaendelea kuratibu usaidizi wa dharura.

Katika ujumbe kwenye Twitter, waziri Mbikayi alitoa pole kwa familia zilizoathirika na mkasa huo.

Hatahivyo Gavana wa jimbo hilo amehoji idadi hiyo ya waziri ya watu waliofariki na kusema kwamba ni watu 10 waliofariki huku wengine takrian 30 wakiwa wamejeruhiwa.

Mbikayi baadaye ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wizara yake inatambua utofuati wa idadi ya waliofariki katika mkasa huo leo na wanajaribu kubaini idadi sahihi.

Duru kutoka shirika la kijamii ameiambia BBC kwamba treni hiyo ilikuwa ni ya mizigo iliyokuwa inasafriki kuelekea mji wa Kalemie.

Mkuu wa operesheni wa kampuni ya kitaifa ya reli nchini Congo, Hubert Tshiakama, ameilezea Reuters kwambamabehewa ya mbele abayo hayakuathirika na ajali hiyo yanaelekea mjini Kalemie.

"Kwa sasa hatuwezi kubaini chanzo cha ajali," amenukuliwa kusema.

Ajali za reli hutokea nchini humo kutokana na miundo mbinu ya kitambo na isiyosimamiza kisawasawa.

Mikasa ya ajali ya treni nchini Congo

2014: Mnamo Aprili takriban watu 63 wamefariki baada ya treni iliyokuwa imebeba abiria kupoteza mwelekeo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la Kamina katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Katanga. Treni hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu kupindukia wengine wakiwa wameketi juu ya treni yenyewe.

2017: Takriban watu 33 wamefariki katika ajali ya treni katika mji wa Buyofwe Kusini mwa jimbo la Lualaba.

2018: Mnamo Novemba, watu 10 waliuawa na wengine kujeruhiwa katika mji wa samba wakati breki za treni ya mizigo zilipokatika.

2019: Zaidi ya watu 20 waliuawa mnamo Machi katika ajali nyingine ya treni iliyopoteza muelekeo katika jimbo la kati la Kasai nchini Congo. Wengine wengi walijeruhiwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii