Mgogoro wa Israel na Palestina: Kwa nini udhibiti wa bonde la Jordan ni muhimu

Tofauti zilizopo kuhusu Bonde la Jordan ni miongoni mwa maswala muhimu katika mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina Haki miliki ya picha COPYRIGHT EMPICS

Waziri mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu alichochea zaidi mgogoro uliopo kati ya taifa lake na Wapalestina kupitia ahadi yake iliozua utata kuhusu kulinyakua bonde la Jordan.

Siku chache kabla ya uchaguzi, waziri mkuu alitoa ofa ambayo inalenga kuomba kura ya wahafidhana katika taifa hilo.

''Iwapo nitapata uungwaji mkono kutoka kwenu ninyi raia wa Israel, natangaza kwamba lengo langu kuhusu serikali mpya kutumia uhuru wetu kulichukua bonde la Jordan pamoja na kaskazini mwa Dead Sea'', alisema Netanyahu.

Tangazo hilo lilisababisha shutuma kutoka kwa Umoja wa Mataifa, mataifa ya Kiarabu na Wapalestina wenyewe.

Kwa nini bonde hilo ni muhimu katika mgogoro kati ya Israel na Wapalestina?

Israel ilikalia ukingo wa magharibi, mashariki mwa Jerusalem, Gaza na milima ya Golan wakati wa vita vya 1967 .

Mwaka 1980 eneo la mashariki mwa Jerusalem lilinyakuliwa na mwaka 1981 milima ya Golan pia ikachukuliwa na Israel.

Hatahiviyo hatua zote hizo hazikutambuliwa kimataifa kwa miongo kadhaa.

Lakini mwaka 2017, utawala wa rais Donald Trump ulibadili sera ya Marekani na kutambua unyakuzi huo wa ardhi ya majirani zake.

Katika hoja zake Netanyahu amechukua hatua mpya akisema kwamba Israel ina fursa kubwa mbele yake kupitia bonde hilo la Jordan.

''Hii ni fursa ya kihistoria na ya kipekee kwa Israel kutumia uhuru wake kuchukua makaazi na maeneo mengine yalio muhimu kwa usalama wetu, turathi na hatma ya siku za usoni''.

Haki miliki ya picha Getty Images

Udhibiti wa ukingo wa magharibi au West Bank ndio kiini kikuu cha mgogoro kati ya Palestina na Israel .

Israel imejenga makaazi 140 katika eneo hilo ambayo yanadaiwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa , ijapokuwa taifa hilo linakana hilo.

Bonde hilo linalopiganiwa, kutoka mji wa Israel wa Beit Shean {kilomita 90 kaskazini mwa Jerusalem} hadi kaskazini mwa Dead Sea , lina ukubwa wa kilomita 2,400 mraba , ikiwa ni thuluthi moja ya eneo lote la ukingo wa magharibi.

Ni ardhi ilio na rutba inayopakana na mpaka wa Jordan. Kuna takriban Wapalestina 53,000 na Wayahudi 12,800 kulingana na Shirika moja la Israel linalopinga ukaliaji huo NGO Paz Now.

Mji wa Palestina katika eneo hilo ni Jericho. Lakini pia kuna miji mengine midogo midogo pamoja na jamii za Bedouin.

Lakini kwa sasa Wapalestina wamepigwa marufuku kuingia katika asilimia 85 ya eneo hilo kulingana na shirika la haki za kibinadamu nchini Israel B'Tselem.

Hatua hiyo ni kwa sababu eneo kubwa lilitajwa kama eneo C chini ya makubaliano ya amani ya Oslo mwaka 1993, ikimaanisha kwamba liko chini ya udhibiti wa Israel, kulingana na Barbara Plett - Usher mwandishi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ijapokuwa makubaliano hayo yalitiwa saini 1993, tangu 1967 bonde hilo la Jordan bado liko chini ya udhibiti wa jeshi la Israel, ambalo limekataa kuondoka katika ardhi hiyo likidai sababu za kiusalama.

''Kulidhibiti bonde la Jordan ni kitu muhimu kwa Israel.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mpaka kati ya Israel na Jordan ni kama mlango wa kuingia mataifa mengine ya mashariki ya kati '', alisema James Sorene, mchanganuzi wa maswala ya Israel, mashariki ya kati na afisa mtendaji wa shirika la mawasiliano na utafiti nchini Uingereza.

"Katika mazungumzo ya mwisho ya amani , bonde hilo lilizua mgogoro mkubwa kwa kuwa Israel bado ilitaka kusalia katika eneo hilo kwa miaka mitano na Paletsina ilitaka kupunguza muda huo . Kulidhibiti eneo hilo kijeshi ndio swala la chini la Israel katika mazungumzo'', alisema Sorene

Ukingo wa magharibi na bonde la Jordan , kulingana na wachanganuzi pia una maana nyingi kwa Wayahudi kwa kuwa baadhi ya turathi zake za kihistoria zilikuwa katika eneo hilo.

Kampeni ya uchaguzi

Uchaguzi wa tarehe 17 mwezi Septemba utakuwa wa pili mwaka huu baada ya ule wa mwezi Aprili ambao Netanyahu hakupata wabunge wengi ili kubuni serikali.

Wakosoaji wa Netanyahu wanaliona pendekezo hilo kama jaribio la kujipatia kura kutoka kwa mrengo wa kulia.

Yair Lapid, kiongozi mwenza wa chama cha Blue and White, alimkosoa waziri mkuu akisema hataki kunyakua ardhi bali anataka kunyakua kura.

"Huu ni ujanja wa uchaguzi na hauna ufanisi wowote kwa kuwa uongo huo uko wazi'', alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images

''Kulinyakua bonde la Jordan pamoja na maeneo mengine yanayokaliwa na Israel katika ukingo wa magharibi ni ahadi za kampeni za uchaguzi. Anazungumzia uhuru , lakini hotuba yake haisemi ni njia gani atakayochukua kutekeleza ahadi hiyo, alisema Sorene. Iwapo atashinda uchaguzi , ahadi hiyo itachukua muda mrefu kutekelezwa''.

Na anaongezea, ''iwapo itatimizwa athari zake zitakuwa mbaya kwa kuwa zitakiuka makubaliano yoyote ya awali''.

''Mpango huo pia unaweza kuvunja makubaliano ya ushirikiano ambapo Netanyahu atahitajika kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas'', alisema Sorene.

Je jamii ya kimataifa inasemaje?

Washirika wa jamii ya kimataifa wameshutumu matamshi hayo ya Netanyahu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa anasema kwamba unyakuzi huo hautahalalishwa katika kiwango cha kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty Images

Muungano wa mataifa ya Kiarabu, shirika linaloshirikisha mataifa 22 , lilitaja mipango ya bwana Netanyahu kuwa hatari na kudai kwamba itavuruga amani katika eneo hilo.

Kwa upande wake waziri maswala ya kigeni nchini Jordan Ayman Safadi alionya kwamba unyakuzi huo huenda ukasababisha ghasia katika eneo lote la mashariki ya kati huku mwenzake wa Uturuki Meylut Cayusoglu akisema kuwa lengo hilo ni la kibaguzi na uchokozi kwa kutumia uchaguzi.

Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh alikuwa amesema kwamba rais wa Israel ni muharibifu wa mchakato mzima wa amani.

Matamshi yake yaliungwa mkono na naibu wa Palestina Hana Ashrawi ambaye aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba ahadi hiyo ya Netanyahu aiharibu uwezekano wa kuwepo kwa mataifa mawili yalio huru bali pia fursa ya amani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii