Tanzania: Chatu mleta ''baraka '' wa Geita ahamishwa

Kundi kubwa la watu wanaofika kumshudia baadhi wakiwa wamebeba zawadi kama vile Mbuzi na Mtama ili kumuomba baraka liliifanya serikali kumhamisha chatu
Image caption Kundi kubwa la watu wanaofika kumshudia baadhi wakiwa wamebeba zawadi kama vile Mbuzi na Mtama ili kumuomba baraka liliifanya serikali kumhamisha chatu

Serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Mali asili na Utaliii imemuondoka nyoka aina ya chatu aliyevuta hisia za wakazi wengi Geita katika pori la kasala ambapo makumi ya watu walifurika kumuona wakiamini ni nyoka wa maajabu. Toka kuonekana kwa nyoka huyo aliyegundulika na wachunga ngombe kumekukuwa na kundi kubwa la watu wanaofika kumshudia baadhi wakiwa wamebeba zawadi kama vile Mbuzi na Mtama ili kumuomba baraka.

"Ndio tunakuja na sisi kutoa sadaka yetu hapa tumeleta mbuzi ili uweze kula, tunajua unameza mbuzi kwa hiyo ameze na tutakuwa tumenusuru wengi" anasema mmoja wa watu waliofika kumshuhudia nyoka huyo.

Mzee Issa Kawandiba aliyeongoza jopo la takribani watu kumi kutoka kijiji cha Kasala anasema kuwa hili ni jambo la kiimani kama vile wengine wanavyo abudu kanisani na msikitini na wao wana abudi chini ya miti maaana wazungu walipokuja walikuta tayari wanamjua mungu na wana namna zao za kuabudu.Mara kadhaa maeneo yenye migodi yamekuwa yakihusihwa na imani hizi ambapo wenyeji wa maeneo hayo wanaamini kwa kufanya matambiko na ibada za namna hii watapata utajiri wa mali. "Unajua haya machimbo yanaenda na 'wakurugenzi' watu wa zamani walioanzisha hizi sehemu sasa yanapofuatwa yale na hizi dhahabu ndio zinatoka" anasema Costansia Joseph.

Image caption Mzee Issa Kawandiba anasema imani ya nyoka ni imani kumhusu sawa na imani nyingine za kidini

Nyoka huyu aliondolewa eneo hilo ambalo maafisa mali asili wanasema yalikuwa ni makazi yake kutokana na kuwepo kwa kiota chake na mayai yake ambayo baadhi yalichukuliwa na wananchi kabla ya kufika kwa maafisa wa mali asili waliomkamata na kumhamishia pori la akiba la Kigosi kwa madai kwamba haikuwa salama nyoka huyo kuendelea kusalia hapo.

Image caption Chatu anayeaminiwa kuleta baraka kwa watu

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii