MV Nyerere: Mwaka mmoja baadaye maisha ya Agustino Cherehani
Huwezi kusikiliza tena

MV Nyerere: Mwaka mmoja baadaye maisha yako vipi kwa fundi Agustino Cherehani?

Kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa kilimo. Mwaka moja uliopita Agustino Cherehani aliyekua fundi mkuu katika kivuko cha MV Nyerere alinusurika kifo katika ajali iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia mbili. Hivi sasa Fundi Agustino Cherehani karejea katika kazi yake ile ile. Kivuko cha MV Nyerere kilipata ajali mkoani Mwanza na kupelekea fundi huyo kukaa ndani ya maji kwa siku tatu kabla ya kuokolewa. Mwandishi wa BBC Eagan Salla amemtembelea Cherehani.

Mada zinazohusiana