Watu 500 waokolewa kutoka jumba la mateso Nigeria
Huwezi kusikiliza tena

Jumba la mateso Nigeria: Polisi wawaokoa watu 500 waliofungwa na kunyanyaswa Kaduna

Wanaume na wavulana 500 wameokolewa kutoka kwenye jumba moja mjini Kaduna ambako walifungwa kwa minyororo na kunyanyaswa kingono Nigeria. Polisi wanasema ni utumwa wa binaadamu. Watu saba wakiwemo walimu katika jumba hilo linalotajwa kuwa shule ya mafunzo ya kidini wamakamatwa.