Vita vya pili vya dunia: Aigundua siri kuhusu kuzaliwa kwake kutokana na mapenzi yaliojiri wakati wa vita

Albert Gilmour with his biological mother Haki miliki ya picha Albert Gilmour
Image caption Albert Gilmour alilelewa akijua mamake ni dada yake mkubwa

Wakati Albert Gilmour alipoitisha cheti za kuzaliwa kwake ili aweze kuoa, mamake alisita kumpatia.

Alipokipata cheti hicho mikononi mwake, kiliifichua siri ya familia.

Mnamo 1965, akiwa na miaka 21 wakai huo, albert aligundua dadake mkubwa ni mamake mzazi.

"Ilikuwa ni hisia ya tamu uchungu," anakumbuka.

Alishtuka kugundua kwamba alilelewa na babu na bibi yake, Albert alimuuliza Ruby Gilmour maswali - "dadake" ambaye kwa hakika alikuwa ni mamake mzazi.

Image caption Wakati Albert alipoomba cheti chake cha kuzaliwa ili aweze kuoa alishtushwa kuona jina la babake haliko

Aliuliza kuhusu babake, ambaye jina lake halikuwepo kwenye cheti hicho, na hakuamini alichoambiwa.

Albert alipewa jina la babake, Albert Carlow, kutoka Calais, Maine - ambaye alikuwa mojawapo ya wanajeshi waliokita kambi Ireland ya kaskazini wakati wa vita vya pili vya dunia.

Ruby alikuwa na miaka 17 alipokutana na mwanajehsi huyo shababu alipokuwa katika kambi liyo karibu na nyumbani kwa kina Ruby, Eglinton, County Londonderry.

Haki miliki ya picha Albert Gilmour
Image caption Albert Carlow na Ruby Gilmour wakati walipokutana wakati wa vita vya pili vya dunia

Wazazi wake Albert walitengana mnamo 1944 msimu wa machipuko wakati babake alipotumwa kwa siri katika fukwa za bahari za Normandy.

Wakati Ruby alipojifungua mwezi Novemba, alimuita mwanawe jina la babake mtoto huyo aliyeamini alikuwa ameuawa vitani.

Kufuatia ufichuzi huo, Albert anasema aliamua kuyaacha kutokana na heshima kwa babu na bibi yake pamoja na mamake.

Lakini takriban miaka 35 baadaye, bintiye Albert Karen Cooke aliamua kufanya utafiti kuhusu familia ya babake kwa siri.

'Habari mbaya'

Alifanikiwa kumpata mojawapo wa mashangazi wake Albert kupitia anuani aliopewana bibi yake Ruby ambayo aliishika kichwani miaka 50 iliyopita.

Albert Carlow alimuandikia mepzni wake anuani hiyo nyuma ya pkiti ya sigara wakati wa vita.

"zawadi nzuri ambayo ningepatia babangu ni kumkutanisha na familia yake," Karen anasema. "Ni sehemu yake ambayo daima nilijuwa imo moyoni mwake, Umarekani."

Haki miliki ya picha Albert Gilmour
Image caption Albert Gilmour aligundua uhalisi wa wazazi wake akiwa na miaka 21

Katika mawasiliano ya usiku sana kwa shangazi yake, alipata habara mbaya kwamba babake alifariki miaka 20 iliyopita.

Lakini Albert alifurahi kusikia kwamba bibi yake mzaa baba bado angali hai na kwamba alikuwa na kaka wawili wa kambo.

Shangazi yake Albert alimpatia picha ya marehemu babake.

Kama picha inavyoonesha , hakuamini ufanano aliokuwa nao na babake.

Haki miliki ya picha Albert Gilmour
Image caption Familia ya Albert Carlow (kushoto) walishtushwa na ufanano na Albert Gilmour (right)

Albert na Karen walisafiri kwenda Marekani kukutana na familia yake ambayo alisema ni kama "ndoto iliojiri kuwa kweli".

"Walisema: ' Tunajua tunapokutazama wewe ni nani, tabia zako, utu wako wewe ni babako mtupu.'

"Sikuwa na haja ya kueleza chochote, sikuhitaji kuthibitisha chochote".

Kwa hisia kubwa Albert alikutana na bibi yake kabla ya kusafiri kwenda kuona kaburi la babake.

Haki miliki ya picha Albert Gilmour
Image caption Albert na bibi yake Belle Carlow walipokutana

Albert aliporudi nyumbani, alimuonyesha mamake Ruby picha ya babake.

"lilia kwa masikitiko, ilikuwa ni vigumu kwake," Albert anasema.

Albert alieleza kwamba babake hakurudi kwa mamake kama alivyoahidi kwasababu alitumwa kwenda Afrika kutoka Ufaransa kabla ya kusafirishwa kurudishwa moja kwa moja nyumbani mwishoni mwa vita hivyo.

Albert anasema alizungumza kwa mara nyingine tena na mamake siku chache kabla ya kufariki kuhusu haya.

"Aliushika mkono wangu na kuniambia: 'Samahani najua nilikupokonya sehemu ya maisha yako'.

"Nilimuambia: 'Huna sabau ya kuomba msamaha'."

Huku akitarajiwa kuingia miaka 75, Albert anasema anataka kuhadithia kuhusu maisha yake binafsi kwa mara ya kwanza.

Anaamini kuna watoto wengine wa wakati wa vita kama yeye "wasiojuwa pa kwenda au wanahisi aibu kulizungumzia".

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii