Iran yamuhukumu kifo''jasusi wa Marekani''

Iranian protesters chant anti-US slogans during a rally in the capital Tehran on 10 May 2019 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tangazo hilo limekuja huku hali ya uhasama ikiendelea kushamiri kati ya Iran na Marekani

Mahakama ya Iran imesema kuwa imewapata na hatia ya kukunya ujasusi watu watatu na kumhukumu mmoja kati yao kifo na mtu mwingine amepatikana na hatia ya kuifanyia ujasusi Uingereza.

Msemaji wa idara ya mahakama Gholam hossein Esmaili ameseam wanaume hao wawili Ali Nafariyeh na Mohammadali Babapour, wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 10- jela kwa kuifanyia kazi shirika la ujasusi la marekani CIA.

Mohammad Amin Nasab amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kulisaidia shirika la ujasusi la Uingereza.

Bwana Esmaili amesema kuwa hawezi kueleza kuwa mtu aliyehukumiwa amehukumiwa kufa kwasababu bado anaweza kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.

Unaweza pia kusoma:

Haijawa wazi ikiwa yeyote miongoni mwa wale waliohukumiwa walikuwa ni miongoni mwa watu 17 ambao wizara ya upelelezi ya Iran ilisema walikuwa wakilifanyia kazi shirika la ujasusi la Marekani CIA mwakaa jana.

Wizara ya ujasusi nchini humo inadai kuwa wamekuwa wakikusanya taarifa kuhusu nyuklia na jeshi pamoja na sekta binafsi - madai ambayo rais wa Marekani Donald Trump aliyapuuzilia mbali na kuyataja kama ''uongo mkubwa''

Bwana Esmaili pia amethibitisha kuwa maafisa wa Iran wamemkamata Muingereza ambaye pia ni Muiran ambaye ni mtaalam wa historia ya binadamu Kameel Ahmady.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Mke wake Kameel Ahmady' alisema kuwa alikamatwa nyumbani kwao magharibi mwa Iran mwezi Agosti

Bwana Ahmady alikuwa akichunguzwa kwa "kuwa na uhusiano na mataifa ya kigeni na taasisi zenye uhusiano na idara za ujasusi za kigeni ", alisema.

Mke wake alisema mnamo mwezi Agosti kuwa alikamatwa magharibi mwa taifa la Iran.

Katika tukio jingine tofauti, vyombo vya habari vya taifa vilimnukuu Bwana Esmaili akitangaza kwamba mahakama ya rufaa kimepunguza kifungo cha kaka yake rais wa Iran Hassan Rouhani kutoka miaka saba hadi mitano.

Hossein Fereydounalikuwa amepatikana na hatia ya "rkupokea hongo", ameamrishwa kurejesha mali alizozichukua , na kupigwa faini ya takriban dola milioni $26.7 , ameongeza Bwana Esmaili

Iliripotiwa mwezi Mei kwamba Bwana Fereydoun, mshauri wa karibu wa rais na mwnadiplomasia , alikuwa amehukumiwa kifungo cha jela ambacho muda wake haukuelezwa bayana kwa kosa la ufisadi.

Wafuasi wa rais wamesema kuwa kesi hiyo ilichochewa kisiasa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii