Harmonize ''ang'ara'' katika tuzo za muziki za MTV Ulaya

Msanii wa bongo Fleva Harmonize Haki miliki ya picha Harmonize/ Facabook

Wiki chache baada ya kujitenga na nembo ya Wasafi -WCB label na kumuoa mpenzi wake Sarah, nyota ya mwanamuziki wa Bongo Flava Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize inaonekana kung'ara hata zaidi.

Harmonise au Konde Boy ameteuliwa kwa ajili ya tuzo ya mwanamuziki bora wa Afrika katika tuzo za muziki za MTV Ulaya ambako anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wanamuziki wa Afrika Kusini Nasty C na Prince Kabyee, Toofan, na Burnaboy.

" Mfalme Kijana wa Muziki Afrika Mashariki , #KondeBoy @harmonize_tz ameteuliwa kwa tuzo kitengo cha mwanamuziki bora wa Afrika 2019 MTV EUROPEAN MUSIC AWARDS," uliandikwa ujumbe wa MTV Africa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Haki miliki ya picha MTV BASE AFRICA/TWITTER

Uteuzi huu unamfanya Harmonize kuwa ndiye msanii wa muziki wa Afrika Mashariki kuwahi kuteuliwa kutoka Afrika Mashasriki na kati.

Iwapo atashinda tuzo hiyo atajiunga na sasa na muajili wake wa zamani katika WCB Diamond Platnumz na AliKiba ambao waliwahi kushinda tuzo hiyo kwa miaka miwili wakifuatana.

Mshindi wa tuzo ya Muziki wa Afrika anapata fursa ya kuendelea katika ngazi ya kimataifa na kushiriki katika kitengo cha muziki wa Asia dhidi ya Muziki wa Afrika.

Unaweza pia kusoma:

Shindano hilo litafanyika Novemba 3 mjini Seville, Uhispani huku mchakato wa kupiga kura ukiwa sasa wazi.

Ariana Grande anaongoza katika orodha ya wanamuziki walioteuliwa akiwa na kura nne, kutoka kwa Mkuu wa Shawn Mendes, Billie Eilish na Lil Nas X wakiwa na uteuzi sita kila mmoja . Lizzo na Taylor Swift kwa pamoja waliteuliwa kwa kura nne.

Hivi karibuni Harmonize aliliandikia kwa kundi la Wasafi Classic Baby WCB akitaka kandarasi yake kuvunjwa.

Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam SK alias Mendez alifichua kwamba msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa.

"Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi," alisema Sallam.

Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo 'My Boo' bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama.

"Sisi kama taasisi ya WCB tuko radhi kwa kile ambacho ataamua, hatuwezi kupinga chochote. Akiamua kufuata maelezo hayo ana baraka asilimia 100 za Wasafi na akitaka kushirikiana na Wasafi wakati wowote tuko wazi. Wajua unapoondoka kwa mazingira mazuri inasaidia uhusiano usalie pale pale," alisema

Haki miliki ya picha Puaz

Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa

"Siku ambayo atatoka kimkataba tutaangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafasi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena," aliongezea Sallam.

Sallam alisema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga.

''Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo''.

''Hatahivyo tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali'', amesema Sallam akinukuliwa na gazeti la Mwananchi Tanzania.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii