Taji la Uhabeshi kurudi nyumbani kutoka Uholanzi lilikofichwa kwa miaka 21

Sirak Asfaw and Arthur Brand sit next to the crown, which depicts the Holy Trinity and Christ's twelve disciples Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Sirak Asfaw, left, and Arthur Brand say they are waiting for the Ethiopian government to get in touch

Taji la Uhabeshi kutoka karne ya 18 linarudishwa nyumbani baada ya kufichwa Uholanzi kwa miaka 21

Raia wa Ethiopia au Uhabeshi Sirak Asfaw, aliyetoroka kwenda Uholanzi katika miaka ya 70 aliligundua taji hilo ndani ya sanduku la mgeni na kutambua kwamba lilikuwa limeibiwa.

Amelilinda kwa wakati wote huu mpaka wakati ambapo amehisi kuwa ni salama kulirudisha.

"Muda umewadia hatimaye kulirudisha taji kwa wamiliki wake - na wamiliki wake ni watu wote wa Uhabeshi," amiambia BBC.

Taji hilo linadhaniwa kuwa mojawapo kati ya 20 yaliopo.

Lina picha ya Yesu kristu Mungu na Roho Mtakatifu, na wafuasi wa Yesu na huenda lilikuwa ni zawadi kwa kanisa kutoka kwa mbabe mwenye nguvu Welde Sellase miaka mia kadhaa iliyopita.

Kwa sasa taji hilo linahifadhiwa katika kituo chenye ulinzi mkali hadi litakaporudishwa nyumbani.

Historia ya taji hilo ni ipi?

Sirak aliondoka nyumbani mnamo 1978 kutoroka ukandamizaji wa kisiasa wa serikali ya kikomyunisti, ilioingia madarakani mnamo 1974.

Utawala huo uliidhinisha wimbi la ghasia zilifahamika kama Red Terror, zilizosababisha kuuawa kwa maelfu ya watu na kuwalazimu wengine wengi kutoroka nchini.

Mkimbizi huyo wa zamani alikuwa mwenyeji wa waethiopia waliotoroka nchini na aliowapokea katika nyumba yake ya kukodi huko Rotterdamkatika miaka ya 1980 na 1990.

"Marafiki, wakimbizi yoyote," anasema. Ilikuwa nimojawpao ya wageni hao walioshukia kwake mnamo 1998 aliyefika akibeba taji hilo kwenye begi lake.

"Watu wengi hawajali kuhusu utajiri hii wa kitamaduni," amesema. " Mimi ni muaminifu kwa Ethiopia."

Sirak alikabiliana na jamaa huyo na kusisitiza kuwa taji hilo halitaondoka hadi iwapo tu liwe linarudi nyumbani.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Taji hilo linahifadhiwa katika kituo chenye ulinzi mkali hadi litakaporudishwa nyumbani.

Baada ya kuomba usaidizi katika majukwa kwenye intaneti - ambayo haikuwa na manufaa yoyote - aliamua kitu cha busarafa ni kuendelea kulihifadhi taji hilo hadi ahisi kwamba ni salama.

"Unaishia katika shinikizo kubwa, hujui umwambie nani au ufanye nini au umkabidhi nani," anasema. "Na pia ukiwa na hofu kwamba serikali ya Uholanzi inaweza kulichukua."

"Niliweka kengele kila mahali nyumbani kwangu za kunijulisha iwapo kuna hatari, nane au kitu kama hivyo.Niliogopa sana!"

lakini kufuaia kumalizika kwa utawala huo wa zamani, na kuchaguliwa kwa waziri mkuu Abiy Ahmed mwaka jana, Sirak amehisi kwamba muda muafaka umewadia kuirudisha historia hiyo ya Uhabeshi nyumbani.

Aliwasiliana na Arthur Brand, anayefahamika kama "Indiana Jones wa sanaa duniani", ili amsaidie kulirudisha nyumbani.

"Nilimueleza, tazama huenda taji au wewe ukapotea ukiendelea hivi," Brand ameieleza BBC.

"Nilimuambia, watu waliohusika wakati huo wakija kujua, hatari iliopo ni kwamba watarudi na wampokonye taji hilo."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Abiy Amed alichaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ethiopia mnamo Aprili 2018

Kwa ridhaa ya polisi ya Uholanzi, Mkusanyaji huyo wa sanaa Brand, aliliweka taji hilo katika eneo salama. Mtaalamu amethibitisha kwamba ni taji halisi na Branda akaamua hatua inayostahili kufuatwa ni kulitangaza wazi.

Wote sasa wanasubiri serikali ya Uhabeshi iwasiliane na maafisa nchini Uholanzi kupanga namna taji hilo litakavyorudishwa.

"Ninataka taji hili liwe ni ishara ya umoja na Upamoja," Sirak anasema. "Tutajivunia taji hili sote Waethiopia kwa pamoja, hata Waafrika."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii