'Maisha yangu kama mchezaji soka mwenye jinsia mbili'
Huwezi kusikiliza tena

James Johnson: 'Jitihada zangu za kuwa mcheza soka mwenye jinsia mbili'

Mshambuliaji wa Nigeria James Johnson, aliyezaliwa na jinsia mbili alianza kucheza katika timu ya soka ya wanawake wakati huo akiitwa Iyabode Abade.

Aliitwa katika kikosi cha taifa cha Nigeria lakini akatimuliwa baada ya wakuu kugundua alikuwa na jinsia mbili.

Baada ya visa kadhaa akiwana miaka 19 Abade aliamua kuwa mwanamume na anajiita James Johnson.

Tangu hapo amezichezea timu za wanaume katika divisheni ya juu Nigeria lakini anasema safari yake haikuwa rahisi.