BBC Africa Eye: Unyanyasaji wa kingono wa wanafunzi
Huwezi kusikiliza tena

Shahada za Ngono: Unyanyasaji wa kingono wa wanafunzi katika Chuo kikuu cha Lagos na Ghana.

Unyanyasaji wa kingono wa wanafunzi wanawake katika vyuo vikuu ni tatizo kote duniani.

Katika mwaka mmoja uliopita BBC Africa Eye imekuwa ikichunguza hali Afrika magharibi.

Wamewahoji wanafunzi kadhaa na kuwatuma waandishi habari wa siri waliojifanya wanafunzi kuwarekodi wanaume wanaowanyanyasa wanawake ndani ya vyuo vikuu viwili vinavyoheshimika kieneo - Chuo kikuu cha Lagos na Chuo kikuu cha Ghana.

Ni lazima tukuonye kuwa taarifa hii ina picha za kuogofya zenye maudhui ya ngono.