Ajuza wa miaka 80 anavyotumia lugha ya mtaani kuvutia wateja
Huwezi kusikiliza tena

Ajuza wa miaka 80 anayetumia lugha ya mtaani kuvutia wateja Tanzania

Wiki ya kwanza ya mwezi October ya kila Mwaka hujulikana kama juma la Huduma kwa wateja.

Wafanyabiashara mbalimbali na hata makumpuni makubwa hutumia siku hizi kuwa karibu zaidi na wateja wao na hata kuwapatia zawadi ili kuzidi kuwavuta kupata bidhaa ama huduma wanazotoa

Lakini umewahi kujiuliza ni kwa namna gani Lugha inavyoweza kumvuta ama kumfukuza kabisa Mteja?

Kutana na ajuza wa Miaka 80 anayetumia Lugha ya mtaani kuvuta wateja kwenye biashara yake

Yeye hufanya nini hasa? Alizungumza na mwandishi wa BBC Scolar Kisanga.

Mada zinazohusiana