Gumzo la #sexforgrades linaendelea
Huwezi kusikiliza tena

#Sexforgrades: Gumzo la unyanyasaji wa kingono vyuo vikuu laendelea kufukuta

Ulimwengu umekuwa ukijadili sakata la unyanyasaji wa kingono katika vyuo vikuu au maarufu mtandaoni kama #sexforgrades kufuatia uchunguzi wa BBC kupitia makala ya Africa Eye katika Vyuo Vikuu vya Lagos na Ghana. Wahadhiri wawili waliotuhumiwa Ghana wamesimamishwa kazi, huku wahadhiri wengine wawili wakisimamishwa kazi katika Chuo Kikuu cha Lagos japo wote wamekanusha madai dhidi yao.