Kikwete akerwa kulishwa maneno ya hotuba yake kwa viongozi wenye utawala wa umwamba

RAIS Haki miliki ya picha Getty Images

Rais mstaafu wa awamu ya nne nchini Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ufafanua kuhusu hotuba yake aliyoitoa Oktoba 8, 2019 katika kongamano la miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere.

Hotuba ya rais mstaafu Kikwete ambayo ilikuwa inawakumbusha viongozi umuhimu wa kujali haki,utu, ukweli, kusikiliza mawazo, uongozi bora na demokrasia ni mambo ambayo mwasisi wa taifa hilo, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anayazingatia.

Neno la 'mwambafai ' limetokana na hotuba hiyo alipokuwa akijadili mada ya "Urithi wa Mwalimu Nyerere Katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa"

Lakini kwa upande wake bwana Kikwete ameamua kutoa ufafanuzi wa barua kuwa hakumlenga kiongozi yeyote mstaafu wala aliyepo madarakani.

Katika hotuba yake, bwana Kikwete alitaja sifa alizokuwa nazo Nyerere akisisitiza kuwa kiongozi ni sawa na mtu mwingine na haimfanyi awe na haki zaidi kuliko wengine.

"Dhamana ya uongozi haikufanyi wewe uwe ni mtu zaidi ya raia wengine wowote waliopo pale. Haikufanyi wewe uwe na haki zaidi kuliko mtu mwingine ambaye si kiongozi. Anao wajibu wake wa uongozi kwako na wewe unao wajibu wako kwa kiongozi wako," alisema Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Image caption Mwalimu Julius Nyerere

"Kinachotushangaza na kutusikitisha sisi ni kujitokeza kwa watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno yaliyosemwa na kiongozi huyu. Wapo wanaojaribu kuweka maneno ambayo hakuyasema," ilieleza barua hiyo.

"Kamwe hakumzungumzia mtu mwingine zaidi ya mwalimu Nyerere ," imeeleza barua kutoka ofisi ya rais mstaafu Kikwete.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii