Kipchoge adai kuvunja rekodi
Huwezi kusikiliza tena

Kipchoge adai kuwa binadamu wa kwanza kukimbia mbio chini ya saa 2

Mashabiki wa michezo nchini Kenya na duniani wanamfuatilia kwa makini mwanariadha wa Kenya, bingwa wa Olimpiki mashindano ya marathon, Eliud Kipchoge kuwa anaweza kuvunja rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili.

Mwanaridha huyo bora zaidi duniani anajaribu kukimbia kwa kasi hiyo katika mashindano yanayotarajiwa kufanyika Vienna nchini Austria mwishoni mwa juma kwa kukimbia dhidi ya muda aliokimbia katika siku za nyuma.

Alimaliza mbio kwa sekundi 26 zaidi ya alivyotarajia katika jitihada ya kwanza ya kukimbia kwa muda wa saa mbili tu huko Monza - Italia.

Mada zinazohusiana