Utafiti wabaini binadamu wa kale Israel walivyohifadhi nyama pangoni

Ngozi iliotolewa kutoka kwa mfupa Haki miliki ya picha PA Media
Image caption Katika uchunguzi wao wanasayasi walipata alama katika ngozi ya mifupa iliohifadhiwa

Wanasayansi nchini Israel wanasema kuwa wamepata ushadhidi kwamba binadamu wa kale walihifadhi nyama kwa lengo la kula siku zijazo.

Ushahidi huo umebainisha kuwa watu walioishi miaka kati ya 200,000 na 420,000 iliopita walikua na uwezo wa kung'amua mahitaji yao ya baadae, wanasema.

Watafiti walichunguza mifupa ya iliyopatikana katika pango la Qesem karibu na mji wa Tel Aviv.

Waligundua alama katika mifupa iliokatwa - iliyoashiria ni mbinu ya kuhifadhi chakula kisiharipike ili iweze kuliwa baadae.

Watafiti wanasema alama hizo iliwekwa kwasababu binadamu wa kale hawakua na uwezo wa kutoa ngozi iliokauka kwenye mfupa uliohifadhiwa kwa muda mrefu.

Alama hizo zilionekana katika 78% ya zaidi ya mifupa 80,000 ya wanyama waliochunguza.

Haki miliki ya picha PA Media

"Mafuta yanayopatikana katika mfupa huwa chanzo muhimu cha lishe bora," alisema Ran Barkai kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv nchini Israel.

"Kufikia sasa, ushahidi umeashiria utumiaji wa mara moja wa korongo kufuatia uchunguzi uliofanyiwa mifuma hiyo baada ya kuondolewa kwa tishu laini'' alisema.

Binadamu wa kale walikua wakiwinda kulungu la mwendo. walihifadhi miguu na fuvu la kichwa cha wanyama hao pangoni na kisha kuondoa mabaki ya mnyama katika eneo alipouliwa,Profesa Jordi Rosell Chuo Kikuu cha Rovira i Virgili nchini Uhispania alisema.

Watafiti walithibitisha kuwa hali katika pango hilo iliruhusu mafuta kwenye mifupa iliohifadhiwa kuwa lishe kwa hadi wiki tisa baada ya mnyama huyo kuuawa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii