Watanzania walalamikia bei ya juu ya mipira ya Kondomu
Huwezi kusikiliza tena

Je, serikali ya Tanzania imefanikiwa katika kukabiliana na uhaba wa mipira ya Kondomu

Nchini Tanzania kwa sasa Serikali inafanya jitihada za kukabiliana na uhaba wa kondomu ulioripotiwa mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo serikali imekwishaingiza nchini humo zaidi ya kondomu milioni 30.

Lakini wasiwasi mkubwa wa wananchi wengi ni kuhusiana na bei ya bidhaa hiyo muhimu kwa kinga ya magonjwa hasa ya zinaa.

Mwandishi wa BBC Gilian Kikowe ametembelea moja ya mitaa huko jijini Dar es salaam, na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Mada zinazohusiana