Ni kwanini kumekuwa na ongezeko la vipodozi miongoni mwa  wanaume?
Huwezi kusikiliza tena

Ni kwanini wanaume wanajipodoa?

Kumekuwa na ongezeko la matumizi ya vipodozi yaani kwa lugha ya wenyewe "Make Ups" katika jamii. Ni jambo la kawaida kwa wanawake hasa wasichana kujipaka vipodozi usoni, kutumia nywele bandia na hata kupanga rangi kucha katika juhudi za kuongezea urembo. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya vipodozi miongoni mwa wanaume yameongezeka na baadhi ya wanajamii wanasema kwamba hii inaenda kinyume cha mila na desturi za kiafrika. lakini je ni kwanini wanawake kwa wnaume wanaonekana kujali sana muonekano wao?. Na je vipodozi ni muhimu kuliko muonekano wa sura halisi ya mtu?. Mwandishi wa BBC Carol Robi amezungumza na mwanaume anayeenzi vipodozi Phillip Mureithi pamoja na Bi Antu Mandoza , mwanamke ambaye haungi mkono matumizi ya vipodozi yeye ni mkereketwa wa muonekano halisia.

Mada zinazohusiana