Ni kweli Zimbabwe inawalazimisha watu kufanya kazi katika migodi ya almasi?

Diamonds Haki miliki ya picha Getty Images

Marekani imepiga marufuku uagizaji wa almasi kutoka Zimbabwe mapema mwezi huu kwa kuhofia watu wanalazimishwa kufanya kazi katika migodi ya madini ya taifa hilo.

Zimbabwe imepuuzilia mbali madai hayo.

Waziri wa habari Nick Mangwana anasema Marekani haina ushahidi wa kuthibitisha madai yake na kuongeza kuwa Washington "imepotoshwa au kuhadaiwa kuhusu"suala hilo.

Eneo la Marange mashariki mwa Zimbabwe linakadiriwa kuwa na hifadhi kubwa ya madini ya almasi duniani.

Madini hayo ni yanasemekana kuwa kiungo muhimu sehemu katika ukuaji wa uchumi wa Zimbabwe.

Zimbabwe's rough diamond exports

$US millions

Source: The Kimberley Process

Maaekani inasema nini What?

Marekani imetaja mfumo wa kuajiri watu katika migodi hiyo imezungukwa na ulaji rushwa na kwamba watu wanaotaka kufanya kazi mahali hapo wanalazimika kulipa hongo kabla ya kuruhusiwa kufika migodini.

Wanapofika, kwa mujibu wa kampuni ya Brenda Smith, wafanyikazi hawaruhusiwi kuoka na wale wnaokaidi amri hiyo wanachukuliwa hatua ya kupigwa/kunyanyaswa kimapenzi ai kukamatwa.

Serikali ya Marekani inasema kuwa ushahidi "umenakiliwa vililivyo".

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Wanajeshi na walinzi wa kibinafsi wanadhibiti migodi ya almasi ya Marange

Ushahidi ni upi?

Wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamedhibitiwa kufika maeneo hayo, lazima wawe na idhini maalum.

Kundi linalochunguza mfumo wa ajira katika migodi ya Marange diamond limekusanya ushahidi kuhusu ajira ya lazima.

Menyekitiwa Bocha Diamond Trust, Moses Mukwada, aliiambia BBC kumekuwa na visa vya wanavijiji kukamatwa na kulazimishwa kufanya kazi katika migodi ya alamasi.

Makundi mengine hata hiyo yalichelea kuzungumzia suala hilo.

Kituo cha kusimamia mali asili (CNRG), shirika la kutetea haki za wachimbaji madini katika eneo hilo, linaasema dhulma dhidi ya wachimbaji madini vinatokana na kufanyishwa kazi kwa lazima.

"Kama shirika hatujapuuza suala la watu [kulazimishwa kazi], lakini taarifa [kutoka kwa serikali ya Marekani]na tungependelea kujua ni nani anamlazimisha nani," Simiso Mlevu, msemaji wa CNRG.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii